• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Askari 1200 waongezwa ili kusaidia kulinda Michezo ya Olimpiki

    (GMT+08:00) 2012-07-25 09:52:25

    Serikali ya Uingereza imeamua kuongeza askari wengine 1, 200, ili kusaidia kulinda usalama wakati wa Michezo ya Olimpiki.

    Katibu anayeshughulikia mambo ya utamaduni, michezo, Olimpiki na vyombo vya habari Jeremy Hunt amesema jana kuwa, uamuzi huo umefikiwa katika mkutano wa kamati ulioongozwa na waziri mkuu wa Uingereza David Cameron.

    Aidha, Hunt amethibitisha kuwa, wanajeshi hao 1, 200 watajiunga na wengine 3, 500 ambao tayari wanaendelea kulinda viwanja ambavyo mashindano hayo ya Olimpiki yatafanyika.

    Mashindano ya Olimpiki ya Kimataifa yanatarajiwa kufunguliwa rasmi ijumaa wiki hii.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako