• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Magwiji wa marathon duniani

    (GMT+08:00) 2012-07-25 18:11:18

    Bendera ya Kenya inatarajiwa kupaa angani wakati wa kinyanganyiro cha mashindano ya olimpiki yatakayoandaliwa jijini la London nchini Uingereza mwezi Julai mwaka huu 2012 katika riadha hususan kwenye mbio za masafa ama Marathon.

    Hii ni kutokana na uzoefu mkubwa walionao wanariadha wa Kenya katika mashindano ya kimatiafa ya riadha kama vile mbio za Afrika IAAF,World Cross Country, na hata mashindano ya dunia ya Olimpiki yanayoandaliwa kila baada ya miaka 5.

    Katika awamu ya kwanza ya makala haya ya riadha tulizungumzia sababu za jiji la Eldoret kuwa chimbuko la wanaraidaha bora duniani, hii leo katika mfululizo wa makala haya tutawazungumzia wanariadha watakaowakilisha Kenya katika mashindano ya Olimpiki.

    Wanariadha tuliokutana nao ni miongoni mwa wale walioteuliwa kuiwakilisha Kenya katika mbio za Marathon kwenye mashindano ya Olimpiki ya London mwaka huu.

    Wao wamewahi kushinda mashindano tofauti ya kimataifa.Wanatusimulia jinsi waliovyojiandaa kuishindia Kenya nishani chungumzima katika Olimpiki pamoja na kuweka historia ya kuwa wanariadha bora duniani.

    Mwanariadha wa kwanza tuliekutana nae asubuhi hiyo ni Abel Kirui,Yeye ni bingwa wa dunia wa Marathon mara mbili.Alishinda mbio hizo mwaka 2009 jijini Berlin Ujerumani na mwaka 2011 katika mji wa Daegu Korea Kusini.

     

    Akiwa kwenye mapumziko kwenye nyumba yake ya kifahari pamoja na mtoto wake na mkufunzi wake, Kirui alielezea furaha yake ya kuteuliwa kuiwakilisha Kenya katika mashindano hayo.Anasema kuwa ana imani kubwa ya kushinda dhahabu na amejianda kwa upinzani kutoka kwa wanariadha wan chi nyingine kama vile Ethiopia.

    Kwa ujuzi wake anasema siri kuu ya ushindi ni kutambua kipawa chako na kujiamini, na fauka ya hayo yeye hufanya mazoezi kwa bidii ya mchwa kila siku ili afanikiwe kukabiliana na wapinzani.

    Tulipooachana na Kirui tulijumuika na mwanariadha wa kike kwa jina Priscah Jeptoo,Yeye ana miaka 28, Priscah ni bingwa wa dunia wa kinadada alieshinda mbio za Marathon za Paris Ufaransa na Turin.Anajivunia mda bora wa saa 2,20 na sekunde 14.

    Alianza kushiriki mbio za kimataifa mwaka 2008.

    Priscah anasema hakudhani kama angeteuliwa kuwa miongoni mwa kikosi kitawachowakilisha Kenya kwenye Olimpiki kwani kulikuwa na upinzani mkali sana upande wa kinadada katika nafasi hiyo.

    Aidha anasema amefanya mazoezi yakutosha na anatarajia kukutana na wasichana wengine wenye ushindani mkali kama vile kama akina Mary Keitany, Edna, Florence, Lucy kabuu na wengine kutoka papa hapa nchini Kenya.

    Ukistaajabu ya Prisach Jeptoo utafurahishwa sana na mwanariadha Edna Kiplagat.Yeye ni bingwa wa dunia wa mashindano ya IAAF ya Marathon mwaka 2011.Edna alijipatia umaarufu mkubwa kwenye mbio za Marathon za Los Angeles na New York Marekani mwaka 2011.

    Zaidi ya hayo kwa sasa anajivunia mda bora wa saa 2 dakika 19 na sekunde 50 baada ya kushinda mbio za London Marathon mwaka huu. Babake Edna alikuwa mwanariadha na yeye ndie aliemhimiza binti yake kukimbia.

    Katika mahojiano yetu, Edna anadokeza kuwa lengo lake kuu ni kuivunja rekodi ya dunia ya wanawake ambayo kwa sasa ni saa 2 na dakika 17. Anasema hakuna siri yoyote ya ufanisi bali kudumisha nidhamu ya hali ya juu na mazoezi makali ndio sababu za ushindi wake.

    Jambo lingine muhimu kuhusu Edna Kiplagata ni kuwa mkufunzi wake wa kibinafsi pia ni mume wake.

    Mwanariadha mwingine tuliefanikiwa kukutana nae katika ziara yetu ni Mary Keitany.msichana alien a umbo dogo sana.Alizaliwa mwaka 1982.Yeye ni bingwa wa dunia wa London Marathon mwaka wa 2012 na anajivunia mda wa saa 2 dakika 18 na sekunde 37.

    Baada ya kushinda mashindano ya London Marathon mwaka huu Mary ana nafasi nzuri sana ya kunyakuwa dhahabu kwenye mbio za Marathon na pia ana mashabiki wingi sana nchini Kenya.

    Mary Keitany akifanyiwa usingaji

    Shirikisho la riadha nchini Kenya AK limeahidi kuwa baada ya maandalizi kabambe na utaratibu muafaka uliotumiwa kuteuwa wanaraidha katika mashindano ya olimpiki ,wana matumaini kuwa Kenya wanariadha hao watabeba bendera ya nchi katika kwa fahari katika mashindano ya Olimpiki na bila shaka watailetea nchi ya Kenya nishani tele na sifa chungu mzima kwa ulimwengu mzima kama kawaida.

    Mwenyekiti wa shirikisho la riadha la Kenya Isiah Kiplagat anasema wamekuwa na mda mgumu wa kuteuwa wanaridha hawa lakini Je uteuzi huo utaleta matunda katika mashindano ya olimpiki ya London Uingereza? Ndilo swali kuu linalohitaji kujibiwa wakati kipenga cha mbio za Marathon za London Uingereza kitakapopulizwa.

    Orodha kamili ya walioteuliwa kwa Marathon upande wa wanaume ni Wilson Kipsang,Abel Kirui na Emmanuel Mutai na upande wa kinadada ni Mary Keitany, Edana Kipalagat na Priscahh Jeptoo.

    Kenya ilishinda medali yake ya kwanza ya dhahabu kwenye mashindano ya marathon ya olimpiki kupitia kwa Samuel Wanjiru aliefariki mwaka 2010.

    Kisu kitakachonolewa zaidi ndicho kitakachochinja ngombe wakati wa mashindano na wavuvi wa pweza hukutana mwambani.tunawatakia kila la kheri wanariadha hawa kutoka Kenya.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako