• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Uzinduzi wa mashindano ya Olimpiki utakuwa na mambo mengi ya kushangaza

    (GMT+08:00) 2012-07-27 10:27:15

    Siri kubwa ya mashindano ya Olimpiki kwa sasa ni jinsi gani uzinduzi wa mashindano hayo utafanyika, lakini kutokana na taarifa zilizotolewa na mamlaka ya Olimpiki na kwa kiasi fulani kuvujishwa na baadhi ya washiriki wa mashindano hayo, uzinduzi huo unatarajiwa kuwa wa kustaajabisha, huku ukiwa na vionjo vya kuwafurahisha watu kwa mtindo wa Uingereza.

    Sherehe hiyo itakayofanyika kwenye uwanja wa Olimpiki, itashuhudiwa na watu 80,000, baadhi yao wakilipia kitita cha paundi 2,012, sawa na dola za kimarekani 3,120, ili kupata viti. Mwongozaji wa sherehe hiyo ni Danny Boyle, mwongoza filamu wa Uingereza ambaye aliongoza filamu maarufu ya Slumdog Millionaire mwaka 2009.

    Moja kati ya kazi za Boyle kwa mwaka 2010, Frankenstein, ilikuwa na kengele kubwa ya kanisani, na wazo hilo limetumika katika sherehe ya uzinduzi wa mashindano hayo, ambapo kengele kubwa zaidi iliyowekwa maalum kwa ajili ya sherehe hiyo, umbali wa kilomita tano tu kutoka uwanja wa Olimpiki, inadhihirisha hilo.

    Kengele hiyo inaendana na wazo la "Kisiwa cha Maajabu" ambalo Boyle analitumia katika sherehe hiyo. Picha mbalimbali za uwanja wa Olimpiki wakati wa uzinduzi zinaonyesha mandhari mbalimbali za kawaida za Uingereza, na kuchanganywa na mandhari za mbuga na mandhari za vijijini.

    Jumla ya watu 25,000 watatumbuiza katika sherehe hiyo, wanyama mbalimbali wanaofugwa pia watakuwepo. Uzinduzi huo umegharimu dola za kimarekani milioni 41.9, na sifa kubwa ya uzinduzi huo, ni jinsi timu 204 zinazoshindana katika mashindano hayo zitakavyoingia katika uwanja huo.

    Sherehe hiyo inatarajiwa kuanza saa tatu kamili za majira ya joto nchini Uingereza, na zitadumu kwa muda wa saa tatu na nusu. Kuingia kwa timu 204 zinazoshiriki mashindano hayo kutachukua muda wa nusu saa.

    Watu wote walioshiriki mazoezi ya uzinduzi huo walitakiwa kutunza siri ya mambo yatakayofanyika, na ni kiasi kidogo tu cha taarifa hiyo kimevuja. Lakini kitu kimoja kimegusiwa mara kwa mara, kwamba sherehe hiyo itakuwa ya kufurahisha na vionjo vya kuwafurahisha watu kwa mtindo wa Uingereza.

    Haijulikani vichekesho hivi vitachukua sura gani, ni vya filamu, futuhi, vichekesho vya haraka, au vya kejeli? Maana vyote hivi ni kawaida ya vichekesho vya Uingereza, lakini mtihani mkubwa ni, je, watazamaji watavifurahia au la?

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako