• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Michezo ya Olimpiki ya London kufunguliwa rasmi leo

    (GMT+08:00) 2012-07-27 16:55:27

    Michezo ya 30 ya Olimpiki ya majira ya joto itafunguliwa rasmi leo tarehe 27 huko London, Uingereza. London ni mji pekee ulioandaa michezo hiyo kwa mara tatu katika historia.

    Nchi na sehemu wanachama 204 wa kamati ya Olimpiki zinazojumuisha wachezaji karibu 11,000 zinashiriki michezo ya Olimpiki ya kimataifa.

    Ripoti iliyotolewa na kampuni ya Brand Finance ya Uingereza inaonesha kuwa, thamani ya nembo ya Olimpiki imeongezeka zaidi na kufikia dola za kimarekani bilioni 47.5, hivyo kuifanya ichukue nafasi ya pili katika orodha ya nembo zenye thamani duniani. Nafasi ya kwanza inachukuliwa na kampuni ya Apple ya Marekani ambayo thamani yake imefikia dola za kimarekani bilioni 70.6.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako