• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Michezo ya Olimpiki yafunguliwa London

    (GMT+08:00) 2012-07-28 18:47:58

    Michezo ya Olimpiki ya majira ya joto imefunguliwa ijumaa usiku mjini London, watu elfu 80 walishuhudia tamasha kubwa la ufunguzi katika uwanja mkuu wa Michezo ya Olimpiki wa London.

    Mlenga shabaha wa China Bibi Yi Siling ametwaa medali ya kwanza ya dhahabu katika michezo ya Olimpiki. Katika mchezo wa kulenga shabaha kwa bunduki mita 10, Bibi Yi alipata ushindi kwa pointi 502.9, na mwenzake Yu Dan alipata medali ya shaba huku mchezaji wa Poland akipata medali ya fedha.

    Michezo hiyo ambayo ni ya 30 inawashirikisha wanamichezo kutoka nchi na sehemu zote wanachama 204 wa Kamati ya Olimpiki ya Kimataifa pamoja na wanamichezo wanne wasiowakilisha nchi au sehemu yoyote. Safari hii ujumbe wa China unaoundwa na wanamichezo 396 utashiriki kwenye michezo 23.

    Wakati wa sherehe za ufunguzi, mwenyekiti wa Kamati ya Olimpiki ya Kimataifa Bw. Jacques Rogge alitoa hotuba akisema, London ni mji pekee ulioandaa michezo hiyo kwa mara tatu katika historia. Ameongeza kuwa timu zote zinazoshiriki kwenye michezo hiyo zinaundwa na wanamichezo wanawake, huu ni msukumo mkubwa wa kuhimiza usawa wa kijinsia.

    Malkia wa Uingereza Elisabeth II alitangaza kufunguliwa rasmi kwa michezo hiyo. Katika siku 16 zijazo wanamichezo zaidi ya elfu 10 watashiriki kwenye michezo mikubwa 26 pamoja na midogo 302. Michezo hiyo itamalizika tarehe 12 Agosti.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako