• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Medali 12 za dhahabu zashindaniwa katika siku ya kwanza ya Michezo ya Olimpiki

    (GMT+08:00) 2012-07-29 20:28:40

    Katika michezo mikubwa 19 iliyofanyika jana kwenye Michezo ya Olimpiki ya London, wanamichezo wa China walijizolea medali nne za dhahabu kati ya 12, na kuvunja rekodi mpya katika mchezo mmoja, na China ikashika nafasi ya kwanza katika orodha ya medali, ikifuatiwa na Italia na Marekani.

    China jana ilipata medali ya kwanza kwenye michezo hiyo kupitia mchezo wa kulenga shabaha kwa bunduki mita 10 kwa wanawake, ambapo mlenga shabaha wa China Yi Siling alinyakua ubingwa huo kwa kupata pointi 502.9, naye muogeleaji wa China Sun Yang alipata ushindi katika mashindano ya kuogelea mita 400 kwa mtindo wa huru kwa wanaume, hii pia ni medali ya kwanza ya dhahabu katika historia ya mchezo wa kuogelea kwa wanaume wa China katika Michezo ya Olimpiki.

    Mwanamichezo mwingine wa China Ye Shiwen alinyakua medali ya dhahabu katika mashindano ya kuogelea mita 400 kwa wanawake kwa kutumia muda wa 4:28:43, na kuvunja rekodi ya Olimpiki ya mchezo huo, ambapo mnyanyua uzito wa China kwa upande wa wanawake Wang Mingjuan alinyakua ubingwa kwenye mashindano hayo kwa kunyanyua uzito wa kilo 48.

    Habari nyingine zinasema, Kamati ya Olimpiki ya Kimataifa jana ilitangaza kumfukuza kwenye Michezo ya Olimpiki mnyanyua uzito wa Albania, Hysen Pulaku kutokana na kushindwa kupitia upimaji wa kujua kama anatumia dawa za kuongeza nguvu au la..

    Leo zinashindaniwa medali 14 za dhahabu katika michezo 24.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako