• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Ikiwa leo ni siku ya nne ya mashindano ya olimpiki jijini London,Uingereza

    (GMT+08:00) 2012-07-31 19:42:22

    Bondia Damien Hooper wa Australia hataaadhibiwa kwa kuvalia fulana yenye bendera ya kabila la Aborigin la nchini humo.Hooper alimshinda Marcus Browne wa Marekani;Mmarekani wa kwanza kushindwa kwenye michezo hiyo.Kamati ya kimataifa ya olimpiki(IOC) imesema haitamchukulia hatua bondia huyo ambaye alikashifiwa vikali na kamati ya olimpiki ya nchini mwake(AOC).Bondia huyo ameongeza kuwa hajali kama atawekewa vikwazo kwani anaona fahari kufanya kitendo hicho ambacho ni cha kutangaza mila zake.Aidha kitendo cha Hooper kinaweza kuchukuliwa kwenda kinyume na kanuni za olimpiki zinazowakataza wanamichezo kutoa matamshi ya kisiasa.

    Muogeleaji Ye Shiwen wa China amekana madai ya utumizi wa dawa za kuongeza nguvu baada ya kuvunja rekodi ya dunia kwenye mashindano hayo.Yi mwenye umri wa miaka 16 alijizolea nishani ya dhahabu kwenye uogeleaji wa miata 400 medley kwa upande wa kina dada na kuivunja rekodi ya dunia kwa zaidi ya sekunde tano.Aidha muogeleaji huyo aliogelea kasi zaidi mita 50 kuliko mshindi kwa upande wa wanaume.Kocha wa Marekani wa timu ya uogeleaji,John Leonard ameutaja ustadi wake wa uogeleaji kama ulojaaa tashwishi.Aidha Leornad ameongeza kuwa ustadi wa Ye unamkumbusha kuhusu waogeleaji wa Ujerumani mashariki katika miaka ya 80 ambapo walikuwa wakitumia dawa za kuwapa nguvu ya kuogelea.Hata hivyo matamshi yake yamelaaniwa vikali na kiongozi wa timu ya Uogeleaji ya China, Xu Qi.Xu amesema kumlinganisha Ye na muogeleaji Lochte wa Marekani hakuna maana yoyote.

    Muogeleaji Ruta Meilutyte wa Lithuania ameishindia nchi yake medali yake ya kwanza ya dhahabu kwenye michezo ya olimpiki.Hii ni baada ya kumlazimisha Rebecca Soni wa Marekani kuchukua nishani ya fedha kwenye uogeleaji mita 100 breaststroke kwa kina dada. Meilutyte mwenye umri wa miaka 15 pia anatarajiwa kushiriki uogeleaji mita 50 na 100 freestyle.Kwenye mchezo huo, Satomi Suzuki wa Japan alitosheka na nishani ya shaba.

    Kijana mmoja ametiwa mbaroni kwa madai ya kumwandikia ujumbe wa wenye maneno maovu mpiga mbizi wa Uingereza, Tom Daley kwenye mtandao mmoja wa kijamii.Daley ambaye babake alifariki kutokana na saratani ya ubongo mwaka mmoja uliopita alipania kutumia olimpiki kushinda medali kama kumbukumbu kwa babake.Aidha mpiga mbizi huyo hakufanikiwa kushinda medali kwenye kitengo alichoshiriki kwa kushika nafasi ya nne.Polisi wamesema kijana huyo aliyetiwa mbaroni alituma ujumbe wa kumkashifu na kumkejeli Daley kwa kushindwa kumtuza babake kwa kushinda medali.

    Timu ya soka ya wanaume ya Uswizi imemtimua mwanasoka Michel Morganella kwa kuandika ujumbe wa kiubaguzi kwenye mtanbdao mmoja wa kijamii.Ujumbe huo uliokuwa unawalenga watu wa Korea Kusini ulianikwa jumapili baada ya Uswizi kufungwa magoli mawili kwa moja na Korea Kusini jumapili iliyopita.Morganella mwenye umri wa miaka 23 tayari amewaommba radhi watu na timu ya Korea Kusini kutokana na ujumbe huo na kutaja kitendo hicho kama kilichotokana na matokeo mabaya ya timu yake.Kocha wa Uswizi, Gian Gilli amesema kitendo cha mwanasoka huyo kimeiabisha nchi hiyo.

    Mpiga makasi wa Niger,Hamadou Djibo Issaka ameshiriki mchezo huo licha ya kuwa na uzoefu wa miezi mitatu wa mchezo huo. Issaka alivutia umati mkubwa wa mashabiki baada ya kumaliza dakika mbili nyuma ya washindi.Mpiga makasi huyo pia alishiriki mchezo huo wenye muda mdogo wa kufuzu ambapo alishika mkia.

    Mama mzazi wa mwanamichezo wa kwanza wa Thailand kushinda nishani kwenye olimpiki amesemekana kujawa na furaha na kupanga kuwa mtawa.Fataki zilitanda angani kwenye kijiji cha mnyanyuaji vyuma, Pimsiri Sirikaew baada ya kushinda medali ya fedha kwenye unyanyuaji vyuma kilo 58 kwa kina dada.Mamake mwanamichezo huyo, Amornat Sirikaew ameviambia vyombo vya habari kuwa alikuwa ameapa kuingia kwenye hekalu la dini ya Buddhha kwa siku tisa iwapo mwanawe angeshinda medali.

    Tuangalie meza ya medali kufikia sasa…..

    JUMLA Dhahabu Fedha Shaba

    1.China 17 9 5 3

    2.Marekani 17 5 7 5

    3.Ufaransa 7 3 1 3

    4.Korea Kaskazini 4 3 0 1

    5.Italia 8 2 4 2

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako