• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Muongeleaji wa China Ye Shiwen apata medali ya pili ya dhahabu

    (GMT+08:00) 2012-08-01 14:41:08

    Ye Shiwen, muogeleaji wa China alitia mkobani nishani yake ya pili ya dhahabu baada ya kushinda uogeleaji mita 200 medley kwa wanawake katika michezo ya Olimpiki ya London.

    Ye alishinda medali yake ya kwanza na kuandikisha rekodi mpya ya dunia kwenye uogeleaji mita 400 medley katika siku ya kwanza ya michezo hiyo. Kwenye uogeleaji mita 200 medley,Alicia Coutts wa Australia alijipatia nishani ya fedha nae Caitlin Leverenz wa Marekani akaridhika na nishani ya shaba.

    Ye alielezea kuhusiana na ushindi huo wa pili. "sikuwa katika hali yangu nzuri leo,nilikuwa nimebakia nyuma kiasi kwenye butterfly,backstroke na breaststroke kwa hivyo nikahitajika kuogelea kutumia mtindo wa freestyle ili kuongeza kasi".

    Wakati huohuo maafisa wa olimpiki wanaendelea kumtetea muogeleaji huyo mwenye umri wa miaka 16 kuhusiana na tetesi za utumizi wa dawa za kumuongezea nguvu.

    Colin Moynihan ni mwenyekiti wa chama cha olimpiki nchini Uingereza. "Ye Shiwen,tunafahamu uwezo wa shirika la kupambana na na utumizi wa dawa(WADA) na limethibitisha kuwa yuko safi na hakuna la zaidi.Ni jambo la kusikitisha kuona kuna dhana nyingi kutoka kwa vyombo vya habari".

    Ye Shiwen ameinua macho ya wengi baada ya kuvunja rekodi ya dunia ya mbio za mita 400 medley na kuogelea kasi zaidi kuliko mshindi kwa upande wa wanaume kwenye kitengo hicho.

    Hali hiyo imepelekea mtangazaji mmoja wa kituo cha televisheni nchini Uingereza BBC na kocha wa timu ya Marekani kukisia utumizi wa dawa za kuongeza nguvu.

    Hata hivyo maafisa wa China wamesema kulinganisha muda wa kina dada na waume si sawa kwani mshindi kwa upande wa wanaume,muogeleaji,Ryann Lochte wa Marekani hakupata upinzani mkali.

    Kufikia sasa hakuna mwanamichezo yeyote wa China aliyepatikana na utumizi wa dawa za kuongeza nguvu katika michezo ya Olimpiki ya London.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako