• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • WBF imefungulia mashataka wachezaji wanane kwa kwenda kinyume na kanuni

    (GMT+08:00) 2012-08-01 20:40:35

    Shirikisho la kimataifa la mchezo wa mpira wa vinyoya(WBF) limefungulia mashataka wachezaji wanane kwa kwenda kinyume na kanuni za mchezo huo.WBF imedai wanane hao hawakujituma kikamilifu kwenye mchezo huo wakiwa na nia ya kuandikisha alama sawa katika michuano ya baadae.Wachezaji hao ni pamoja na Wang Xiaoli na Yu Yang wa China, Greysia Polii na Meiliana Jauhari wa Indonesia, Jung Kyung Eun,Kim Ha-na, HA Jung-eun naKim Min Jung wa Korea Kusini.Watazamaji waliwazomea na kuwatupia maneno ya matusi wachezaji hao walipokuwa wakionekana wazi kuenda kinyume na kanuni ili kujipatia alama sawa.

    Mwanamichezo wa Brazil wa mchezo wa judo, Felipe Kitadai ameivunja medali yake ya shaba kwa bahati mbaya alipoiangusha chooni. Kitadai amesema sehemu inayoshikilia medali hiyo imevunjika hivyo hawezi kuivaa shingoni.Mwanamichezo huyo alishinda nishani hiyo ya shaba kwenye mchezo wa judo kilo 60 kwa wanaume wikendi iliyopita.Kamati ya olimpiki ya Brazil imedokeza kuwa itaomba medali mpya ijapokuwa inafahamu kuwa kamati ya kimataifa ya olimpiki(IOC) haina jukumu hilo.

    Kamati ya olimpiki ya Brazil(BOC) imelaani vikali ile imekiita "maoni ya kiubaguzi" yaliyoelekezewa mwanamichezo wake wa mchezo wa Judo, Rafaela Silva.BOC imesema maoni hayo yaliyoelekezewa mwanamichezo huyo yaliandikwa kwenye mtandao mmoja wa kijamii.Aidha BOC imedai maoni hayo yaliandikwa pale Silva alipoondolewa kwenye robo fainali ya kitengo cha kilo 57 kwa kina dada na Miryam Roper wa Ujerumani.Hata hivyo Silva amedokeza kuwa hana nia ya kuchukua hatua dhidi ya maoni hayo huku BOC ikisema inashauriana ili kuchukua hatua za kisheria dhidi ya aliyeandika maoni hayo.

    Mwanamichezo wa Afrika Kusini wa mchezo wa kulenga kupiga mshale kwa upande wa kina dada, Karen Hultzer amezungumzia kwa mara ya kwanza kuhusu jinsia yake.Kwenye mahojiano na mtandao mmoja, Hultzer amekiri kuwa yeye ni msagaji.Aidha mpigaje huyo mshale amesema imembidi kuweka wazi swala hilo kwa sasa kwani hakutaka kusumbuliwa na vyombo vya habari wakati akishiriki mchezo huo. Hultzer alishindwa kwenye mchezo huo na Pia Lionetti wa Italia.Mtandao huo uliomfanyia mahojiano Hultzer umejikita sana kuangazia wanamichezo wasagaji na mabasha kwenye mashindano hayo ya olimpiki jijini London.

    Mke wa Kobe Bryant;mwanakikapu wa timu ya Marekani amesemekana kupandwa na hasira na kuona aibu baada ya picha za mumewe akiwa kifua wazi na kukaa katikati ya wanawake wawili kusambaa kwenye mitandao.Bryant na timu ya kikapu ya Marekani walikuwa wamekwenda mjini Barcelona,Hispani kusherehekea ushindi wao. Vanessa anadaiwa kukasirishwa na kitendo hicho zaidi ikizingatiwa wawili hao walipania kupeana talaka kabla ya kuamua kusuluhisha matatizo yao.Taarifa zinadokeza kuwa Vanessa anaamini mumewe hakuhusika kimapenzi na vipusa hao lakini hakupendezewa na kuwa kwake kifua wazi karibu nao.Hata hivyo mtandao mmmoja umetoa taarifa kusema kuwa jamaa mmoja alimmwagia maji Bryant bila kukusudia hivyo akawa anasubiri kupewa fulana nyingine.

    Jo-Wilfried Tsonga wa Ufaransa amemshinda Milos Raonic wa Canada na kufikia raundi ya tatu kwenye mchezo wa tenisi kwa wanaume uliochukua muda mrefu zaidi kwenye historia ya olimpiki. Tsonga alishinda kwa kutumia saa tatu dakika 56.

    Tuangalie meza ya medali kufikia sasa…..

    JUMLA Dhahabu Fedha Shaba

    1.China 23 13 6 4

    2.Marekani 23 9 8 6

    3.Ufaransa 11 4 3 4

    4.Korea Kusini 8 3 2 3

    5.Korea Kaskazini 4 3 0 1

    10.Afrika Kusini 2 2 0 0

    25.Misri. 1 0 1 0

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako