Takwimu zilizotolewa tarehe 3 na wizara ya mambo ya umma na ofisi ya kamati ya kupunguza hasara za maafa ya China zinaonesha kuwa, vimbunga vya Saola na Damrey vimewalazimisha watu laki 5.49 wa mikoa minne ya China ikiwemo Jiangsu, Zhejiang, Fujian na Shandong kuhama kwa muda makazi yao.
Ili kukabiliana na vimbunga hivyo viwili, ofisi ya kamati ya kupunguza hasara za maafa ya China ilitoa tahadhari julai 31 na kupanga kazi za kuzuia maafa ya dharura. Idara za mambo ya umma za mikoa minne ya Jiangsu, Zhejiang, Fujian na Shandong pia zimetoa tahadhari, na kutuma makundi vya wafanyakazi kwenye sehemu zinazoweza kuathiriwa zaidi na vimbunga hivyo, ili kusaidia kazi ya kukabiliana navyo, na kutoa msaada wa mahema na mifarishi kwa watu walioathiriwa.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |