• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Siku ya 11 kwenye mashindano ya olimpiki jijini London

    (GMT+08:00) 2012-08-07 19:24:30

    Raia wa nchi ya Greanada iliyoko kwenye visiwa vya Caribbean wameingia kwenye sherehe baada ya mwanariadha wa nchi hiyo,Kirani James kujinyakulia medali ya dhahabu kwenye mbio za mita 400 kwa wanaume.Waziri Mkuu wa nchi hiyo,Tillman Thomas amemtaja mwanariadha huyo kama mfano bora kwa vijana wa Grenada,nchi yenye idadi ya watu laki moja.James mwenye umri wa miaka 19 amekuwa mwanariadha wa kwanza ambaye si raia wa Marekani kukimbia chini ya sekunde 44 kwenye mbio hizo.Mwanariadha huyo alitumia sekunde 43.94 na kutangazwa bingwa wa dunia.Aidha serikali ya Grenada imetangaza siku ya leo mchana kama sikukuu ya kitaifa kutokana na ushindi wa mwanariadha huyo.

    Refarii wa mchezo wa mpira wa wavu wa ufukweni(Beach Volleyball) Darryl Friesen wa Canada alibidi kuacha kusimamia mechi kati ya timu ya Ujerumani na Brazil baada ya kuugua.Aidha refarii huyo aliondolewa uwanjani na watabibu dakika 20 baada ya mechi hiyo kuanza.Reafrii wa pili wa mechi hiyo, Wang Leijun wa China alichukua jukumu la kusimamia mechi hiyo baada ya Friesen kuondolewa kiwanjani.Msemaji wa shirikisho la kimataifa la mchezo huo(FIVB), Dominic Clark amesema kuwa refarii huyo alikuwa anashiriki olimpiki yake ya nne.

    Kocha wa timu ya mpira wa kikapu ya Uingereza ya wanaume, Chris Finch amejiuzulu.Hii ni baada ya timu hiyo kuondolewa kwenye mashindano hayo.Timu hiyo ya wanaume ilishinda mechi moja kati ya tano ya kundi lake kwenye mashindano hayo ya olimpiki.Finch ambaye ni naibu kocha wa timu ya mpira wa kikapu ya Houston Rockets nchini Marekani.

    Mwanamichezo Nicholas Delpopolo wa Marekani amefurushwa kutoka mashindano ya olimpiki jijini London.Hii ni baada ya kutopita majaribio ya upimaji na kukiri kutumia chakula kilichochanganywa na bangi. Delpopolo mwenye umri wa miaka 23 anayeshiriki mchezo wa judo kitengo cha kilo 73 alimaliza katika nafasi ya saba kwewnye mchezo huo.Aidha Delpopolo alifurushwa na bodi ya kimataifa ya Olimpiki(IOC) baada ya kugundua chembechembe za bangi kwenye haja ndogo.Mwanamichezo huo alipimwa punde baada ya kupoteza pigano lake dhidi ya Nyam-Ochir Sainjargal wa Mongolia.Ioc imetaka jina la Delpopolo kuondolewa kwenye rekodi za jijini London na kupendekeza shirikisho la kimataifa la Judo(IJF) kumpa adhabu.Hata hivyo Delpopolo ameomba radhi kwa kamati ya olimpiki ya Marekani na wanamichezo wenzake.

    Mwanamichezo wa Marekani, Steven Lopez amesema anataka kushinda nishani ya dhahabu ya mchezo wa taekwondo jijini London.Lopez alishinda nishani ya shaba kwenye olimpiki ya mwaka 2008 jijini Beijing, China.Aidha dadake mdogo,Diana pia anasaka nishani ya dhahabu ya mchezo huo kwa kina dada na kuwa chini ya kocha Jean ambaye ni kaka yao.Diana ambaye pia alishinda medali ya shaba kwenye olimpiki jijini Beijing ameonyesha ari kama ya kakake kuweza kushinda medali ya dhahabu.Steven,Diana na kaka yao Mark;ambaye hakufuzu mwaka huu, waliandikisha hitoria kwenye olimpiki ya Beijing kwa kuwa ndugu watatu wa kwanza kujumuishwa kwenye timu ya Marekani tangu mwaka 1904.Mchezo huo wa taekwondo uligonga vichwa vya habari kwenye olimpiki ya Beijing baada ya mwanamichezo Angel Matos wa Cuba kumpiga teke usoni refarii baada ya kuondolewa.

    Mwanariadha Kim Collins wa kisiwa cha St. Kitts aliondolewa kwenye timu ya nchi yake baada ya kulala na mkewe hotelini.Taarifa zinadokeza kuwa mwanariadha huyo alikuwa ashiriki mbio za mita 100 kwa wanaume.Hata hivyo Collins alisema hajutii kitendo hicho kwani hawezi kumwacha mkewe na kuchagua timu hiyo.

    Timu ya Hispania ya wanaumme ya mchezo wa mpira wa kikapu,imekana madai kuwa ilifanya kusudi kufungwa na Brazil ili kuhepa mchuano wa nusu fainali dhidi ya Marekani.Hispania iliyofungwa vikapu 88-82 na Brazil hawatakutana na Marekani iwapo watafikia hatua ya nusu fainali.Madai haya yanajiri siku kadha baada ya wachezaji wa wane wa mchezo wa mpira wa vinyoya kufurushwa baada ya kuonekana kutojituma kushinda mechi zao.

    Tuangalie meza ya medali kufikia sasa…..

    JUMLA Dhahabu Fedha Shaba

    1. China 64 31 19 14

    2. Marekani 63 29 15 19

    3. Uingereza 40 18 11 11

    4. Korea Kusini 22 11 5 6

    5. Ufaransa 26 8 9 9

    16. Afrika Kusini 4 3 1 0

    27. Ethiopia 4 2 0 2

    31. Kenya 5 1 2 2

    42. Misri 2 0 2 0

    47. Tunisia 2 0 1 1

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako