• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Siku ni ya 12 ya mashindano ya olimpiki jijini London,Uingereza

    (GMT+08:00) 2012-08-08 18:13:11

    Maafisa wa timu ya olimpiki ya Cameroon wamesema wanamichezo saba wamepotea wakiwa nchini Uingereza kwa mashindano hayo.Mkuu wa timu hiyo, David Ojong ameongeza kuwa saba hao ambao walitoweka wikendi iliyopita ni pamoja na mabondia watano,muogeleji na mwanasoka wa kike.Sababu za kutoweka kwao hazijajulikana lakini tetesi zinadai kuwa wanataka kusalia nchini Uingereza kutokana na matatizo ya kiuchumi nchini mwao.Hili si tukio la kwanza kwenye michezo hiyo ikiwa ni mwezi mmoja tangu ubalozi wa Sudan utangaze kutoweka kwa wanamichezo wake watatu.Tayari mmoja amesemekana kujiandikisha kutafuta hifadhi nchini Uingereza na wengine wawili wakitarajiwa kuchukua hatua kama hiyo.

    Muogeleaji bingwa wa mita 100 Breastroke kwa wanaume, Cameron van der Burgh wa Afrika Kusini amekiri kudanganya kwenye ushindi wake ulionukuliwa kama rekodi ya dunia.Kwenye kitengo cha Breastroke muogeleaji hutakiwa kutumia mtindo mmoja wa pomboo kuchapa maji mara moja anapoanza na kugeuka wakati wa uogeleaji.Aidha kwenye video ya marudio van der Burgh ameonekana akitumia mtindo huo mara tatu kutokana na ukosefu wa kamera za chini ya maji.Akiongea na gazeti moja muogeleaji huyo amekiri kuvunja sheria na kuongezea kuwa waogeleaji wengi hutumia mbinu kama hiyo.Hii si mara ya kwanza kwa mtindo huo wa kuchapa maji wa pomboo kuzua hoja kwenye uogeleaji wa kitengo cha Breaststroke.Muogeleaji Brenton Rickard wa Australia aliyenyakua nishani ya fedha pia alionekana akitumia mtindo huo mara mbili alipoanza kuogelea.

    Mwanariadha Asafa Powell wa Jamaica hatajumuishwa kwenye kikosi cha nchi hiyo kutetea taji la mita 400 kwa wanaume kupokezana kijiti.Hii ni baada ya mwanariadha huyo kupata jeraha la kiuno ambalo kulingana na daktari wake litachukua muda wa wiki tatu kupona.Powell mwenye umri wa miaka 29 aliumia wakati wa fainali ya mbio za mita 100.Aidha wanariadha Usain Bolt, Yohan Blake, Nesta Carter and Michael Frater ndio wanaotarajiwa kuinua hadhi ya Jamaica kwenye mbio hizo jumamosi hii.Kutokana na jeraha hilo Powell hatoshiriki tena riadha msimu huu na kusema atajitokeza tena mwakani.

    Wakati huohuo,bingwa wa mbio za mita 100 kwa wanaume,Usain Bolt wa Jamaica amesema angependa kujiunga na timu moja ya soka kwenye ligi ya nchini Uingereza.Bolt amesema hafanyii masihara swala hilo na endapo kocha wa timu ya Manchester United,Sir Alex Fergussona atamwita kufanya majaribio hatakataa ombi hilo.Aidha mwanariadha huyo amempa changamoto kocha huyo wa Manchester United kumtafuta katika siku chache ambazo yupo jijini London.

    Aliyekuwa nahodha wa timu ya mchezo wa magongo ya Pakistan, Islahuddin Siddique ameelezea wasiwasi wake kuhusiana na siku za mbeleni za mchezo huo nchini mwake.Hii ni baada ya timu ya Pakistan ya mchezo huo kukubali kipigo cha magoli saba bila jawabu kutoka kwa Australia hivyo kuyaaga mashindano hayo ya olimpiki.Aidha Siddique ameongeza kuwa anazidi kusikitishwa na kudorora kwa mchezo huo nchini mwake ikiwa Pakistan ilimaliza ya mwisho kwenye kundi lake kwenye mashindano ya dunia mwaka 2010.Pakistan imewahi kushinda medali kwenye mchezo huo mwaka 1960, 1968 na 1984.

    Mlolongo wa mabondia wamaoendelea kukata rufaa kutokana na uamuzi kwenye michezo ya olimpiki unazidi kuwa mrefu.Wanamasumbwi kutoka Ufaransa na Canada wamewasilisha rufaa zao kuhusiana na sare kwenye robo fainali ya kitengo cha uzani wa welter.Aidha maombi ya mabondia hayo yametupiliwa mbali huku uadilifu wa chama cha kimataifa cha ngumi(AIBA) ukitiliwa shaka.Bondia Alexis Vastine wa Ufaransa aliitupa chini kwa hasira na kuivunja chupa ya maji baada ya refarii kumtangaza bondia Taras Shelestyuk wa Ukraine kama mshindi.

    Tuangalie meza ya medali kufikia sasa…..

    JUMLA Dhahabu Fedha Shaba

    1. China 73 34 21 18

    2. Marekani 70 30 19 21

    3. Uingereza 48 22 13 13

    4. Korea Kusini 23 12 5 6

    5. Russia 48 10 18 20

    18. Afrika Kusini 4 3 1 0

    27. Ethiopia 4 2 0 2

    32. Kenya 5 1 2 2

    38. Algeria 1 1 0 0

    42. Misri 2 0 2 0

    49. Tunisia 2 0 1 1

    65. Morocco 1 0 0 1

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako