• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Siku ni ya 14 kwenye mashindano ya olimpiki jijini London,Uingereza.
    Siku moja imesalia kwa mashindano hayo kukamilika.

    (GMT+08:00) 2012-08-11 19:46:34

    Tuanze na riadha mbio za mita 5000 kwa kina dada ambapo mwanariadha Meseret Defar wa Ethiopia alitimua vumbi na kuibuka na nishani ya dhahabu na kumlazimsha Vivian Cheruiyot wa Kenya kuchukua medali ya fedha na mwanariadha raia mwenza,Tirunesh Jibaba akajitwika nishani ya shaba.Kwenye mbio za mita 1500 kwa kina dada,Asli Cakir na Gamze Bulut wa Uturuki walichukua nishani za dhahabu na fedha mtawalia na kumwacha Maryam Jamal wa Bahrain kujiwalaza na medali ya shaba.Bado kwenye riadha timu ya Marekani ya kina dada ya mbio za mita 400 kupokezana kijiti ilijinyakulia nishani ya dhahabu na kuandikisha rekodi mpya ya dunia.Jamaica ilijivika nishani ya fedha nayo Ukraine ikajiliwaza na nishani ya shaba.

    Tujitose kwneye maji makuu ambapo Mellouli Oussama wa Tunisia alitia mkobani nishani ya dhahabu kwenye mchezo wa kuogelea baharinii kwa wanaume na kuwalazimisha Lurz Thomas wa Ujerumani na Weinberger Richard wa Canada kujichukulia medali za fedha na shaba mtawalia. Oussama ameingia kwenye vitabu vya historia ya olimpiki kwa kuwa muogeleji wa kwanza kushinda medali kwenye kuogelea kidimbwini na baharini.

    Mchezo wa uendeshaji mashua wa timu ya watu wawili kwa wanaume kitengo cha 470 ulishuhudia Belcher Mathew na Page Malcolm wa Australia wakibeba medali ya dhahabu, Patience Luke na Bithell Stuart wa Uingereza wakajitwika medali ya fedha nao Calabrese Lucas na de la Fuente Juan wa Argentina wakachukua nishani ya shaba.kwa upande wa kina dada, Aleh Jo na Powrie Olivia wa New Zealand walivikw nishani ya dhahabu, Mills Hannah na Clark Saskia wa Uingereza wakajichukulia nishani ya fedha nao Westerhof Lisa na Berkhout Lobke wa Uholanzi wakajiliwaza na medali ya shaba.

    Timu Russia ya kina dada ilijichukulia medali ya dhahabu kwenye uogeleaji wa sarakasi,China ikavikwa medali ya fedha nayo Hispania ikakumbati nishani ya shaba.

    Mchezo wa mpira wa magongo kwa kina dada ulishuhudia timu ya Uholanzi ikibeba nishani ya dhahabu baada ya kuwafunga mabingwa wa dunia,Argentina mali mawili kwa sufuri na kuwalazimisha kuchukua medali ya fedha.Aidha Uingereza iliifunga New Zealand magoli matatu kwa moja na kuvikwa medali ya shaba.

    Pajon Mariana alivikwa nishani ya dhahabu kwenye uendeshaji baiskeli aina ya BMX kwa kina dada, Walker Sarah wa new Zealand akaikumbatia medali ya fedha nae Smulders Laura wa Uholanzi akatosheka na nishani ya shaba.Kwa upande wa wanaume, Strombergs Maris wa Latvia alichukua medali ya dhahabu, Willoughby Sam wa Australia akajitwalia medali ya fedha nae Oquendo Zabala Carlos Mario wa Colombia akaridhika na nishani ya shaba.

    Lavillenie Renaud wa Ufaransa alijinyakulia nishani ya dhahabu kwenye mchezo wa kuruka kutumia upondo kwa wanaume,Otto Bjorn na Holzdeppe Raphae wa Ujerumani wakavikwa nishani za fedha na shaba mtawalia

    Kwenye mchezo wa mieleka kwa wanaume freestyle wa kilo 55, Otarsultanov Dzhamal wa Russia alinyanyua medali ya dhahabu, Khinchegashvili Vladimer wa Georgia akachukua medali ya fedha nae Yang Kyong Il wa Korea Kaskazini na Yumoto Shinichi wa Japan wakagombania nishani ya shaba.Bado kwenye mieleka kwa wanaume kitengo cha kilo 74 freestyle,Jordan Burroughs wa Marekani alibeba nishani ya dhahabu baada ya kumshinda Sadegh Saeed Goudarzi wa Iran..Hii ni medali ya kwanza ya dhahabu kwa Marekani kwenye mchezo huo.

    Lysenko Tatyana wa Russia alivikwa medali ya dhahabu kwenye mchezo hammer kwa kina dada, Wlodarczyk Anita wa Poland akachukua medali ya fedha nae Betty Heidler wa Ujerumani akakumbati medali ya shaba.

    Tuangalie meza ya medali kufikia sasa…..

    JUMLA Dhahabu Fedha Shaba

    1. Marekani 94 41 26 27

    2. China 81 37 25 19

    3. Uingereza 58 26 15 17

    4. Russia 64 15 21 28

    5. Korea Kusini 27 13 7 7

    21. Afrika Kusini 5 3 1 1

    22. Ethiopia 6 3 0 3

    36. Kenya 8 2 3 3

    40. Tunisia 3 1 1 1

    45. Algeria 1 0 0 1

    51. Misri 2 0 2 0

    64. Botswana 1 0 1 0

    75. Morocco 1 0 0 1

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako