• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wajumbe 2,270 wamechaguliwa kuhudhuria mkutano mkuu wa 18 wa CPC

    (GMT+08:00) 2012-08-13 20:05:38

    Jumla ya wajumbe 2,270 wamechaguliwa kuhudhuria mkutano mkuu ujao wa 18 wa Chama Cha Kikomunisti cha China (CPC).

    Taarifa rasmi iliyotolewa leo imesema, rais Hu Jintao na wajume wengine 8 wa kudumu wa Ofisi ya siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China wanatarajiwa kuhudhuria mkutano huo.

    Wajumbe wengine 50 zaidi watahudhuria mkutano huo wa 18, hili ni ongezeko la wajumbe kuliko mkutano mkuu wa 17 wa CPC miaka mitano iliyopita. Wajumbe hao wamechaguliwa kutoka sehemu mbalimbali nchini China wakati wa mikutano ya chama katika mikoa mbalimbali. Wajumbe hao wanapaswa kupita vigezo vilivyowekwa ili kuweza kupata kibali cha kuhudhuria mkutano huo.

    Zaidi ya wanachama milioni 82 wa Chama cha Kikomunisti cha China watawakilishwa na wajumbe watakaohudhuria mkutano mkuu wa 18 wa chama hicho, ambao unatarajiwa kufanyika katika nusu ya pili ya mwaka huu hapa Beijing.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako