Hali ya wasiwasi bado imeendelea kuwepo mjini Mombasa, wakati maandamano kufuatia kuuawa na watu wasiojulikana kwa mtuhumiwa wa ugaidi Sheikh Aboud Rogo Mohammed jumatatu mchana. Ofisa mmoja wa polisi aliuawa jana mjini humo wakati alipokuwa akiwatawanya vijana waliokuwa wanafanya fujo na kuchoma moto kanisa moja katika mtaa wa Kisauni. Askari wengine wanne walijeruhiwa baada ya vijana hao kuwarushia guruneti.
Mwendesha mashtaka mkuu wa Kenya Teriako Tobiko ameagiza polisi kuyafanya uchunguzi mara moja kuhusu kuuwa kwa Rogo, na kuwasilisha ripoti ndani ya wiki mbili. Awali, viongozi wa waumini wa dini ya kiislamu waliokutana jijini Nairobi waliilaani serikali kwa kuhusika na mauaji ya Sheik Rogo, wakiuliza ni kwa nini hakuna mtu aliyekamatwa baada ya mauaji kutokea wakati wa mchana.
Wakati huohuo polisi wa Kenya wamelihusisha kundi la Al-Shabaab lililo na uhusiano na kundi la kigaidi la al Qaida na mauaji ya Sheikh Rogo. Naibu msemaji wa polisi wa Kenya Bw Charles Owino amesema kutokana na vurugu zinavyoendelea na guruneti lilivyotumiwa kwa ufanisi, inaonesha kuwa kuuwa kwa sheikh Rogo kulipangwa kwa makini.
Kundi la Al-Shabaab linahusika na utekaji wa wageni na mashambulizi kadhaa yaliyotokea mwishoni mwa mwaka jana na kupeleka Kenya kutuma vikosi nchini Somalia kupambana na kundi hilo.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |