• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • barua 0731

    (GMT+08:00) 2012-08-29 15:32:00
    Barua ya kwanza inatoka kwa Geoffrey Wandera Namachi wa Eveready Security Guard S.L.P 57333 Nairobi Kenya anaanza kwa kusema mwaka wa 2011 umekamilika kitambo, mwaka huo unapokamilika umeacha nyuma historia ambayo imekusanywa na kuingia kwenye daftari za kumbukumbu duniani. Miongoni mwa taarifa kuu zilizopewa uzito ni kuuawa kwa gaidi mkuu duniani Osama bin-Laden pamoja na mshirika wake Bwana Fazul Abdullah Mohammed ambaye alikuwa kiongozi wa mtandao wa kigaidi katika kanda hii ya Afrika Mashariki.

    Habari nyiongine ni kuhusu kifo cha Muammar Gaddafi ambaye aliongoza nchi ya Libya kwa kipindi cha miaka 40 hatimaye aliuawa. Mbali na vifo tukio jingine lilitokea mwanzoni mwa mwaka 2011 ni Tsunami kali iliyotokea nchini Japan na kusababisha uharibifu mkubwa wa miundo mbinu na majeruhi kadhaa. Ufichuzi wa mtandao wa wikileak ambapo tulipokea habari nyingi kuhusu nchi ya Amerika na nchi nyingine duniani hususana ubalozi wa Amerika.

    Hatimaye aliyekuwa rais wa Misri Hosni Mubarak alitimuliwa madarakani kupitia maandamano ya wananchi, Mubaraka alitawala nchi hiyo kwa kipindi cha miaka 30. Kenya na Tanzania hazitasahauliwa kutokana na mikasa iliyotokea, ambapo Kenya ilipatwa na mkasa wa moto, huku Tanzania ikipatwa na mkasa wa meli kuzama. Licha ya hayo kwa mara ya kwanza dunia ilishuhudia kuchaguliwa kwa mwanamke kuliuongoza shirika la IMF Bibi Christine Lagarde mzaliwa wa Ufaransa.

    Pamoja na hayo bara la Afrika hususana Afrika Mashariki pamoja na dunia nzima ilishuhudia kuzaliwa kwa nchi changa barani Afrika yaani Sudan Kusini mnamo tarehe 9 mwezi wa 7. kwa sasa nchi hiyo imekuwa ya 193 ulimwenguni na nchi ya 54 barani Afrika. Hivyo ni baadhi tu ya vidokezo vya matukio yaliyogonga vichwa vya habari duniani. Mwisho naipa redio China Kimataifa mkono wa pongezi kwani imeniwezesha kufahamu matukio kutoka pembe zote ulimwenguni, ndiyo maana nasema CRI ndiyo kituo changu, naitakia CRI kila la kheri katika mwaka huu wa 2012.

    Tunakushukuru sana msikilizaji wetu Geoffrey Wandera Namachi kwa barua yako iliyojaribu kudondoa matukio kadhaa ya mwaka jana. Mwaka uliopita ulikuwa na matukio makubwa sana, ingawa baadhi yao yamejirudia tena kama vile kuzama kwa meli nchini Tanzania. Tunatumai kuwa katika kipindi kilichosalia cha mwaka huu hakutatokea matukio makubwa ya kusikitisha. Ahsante sana.

    Barua nyingine inatoka kwa msikilizaji wetu Amos Msanga, baruapepe yake ni amosmsanga@rocketmail.com, anasema suala la mazingira katika maeneo mengi hasa Afrika katika maeneo ya vijijini limeendelea kuwa gumu kwani kila leo miti, mimea, maji na wanyama vinaendelea kuteketezwa. Naoimba serikali iliangalie suala la mazingira na udhibiti wake kabla vijiji havijawa na majangwa katika vizazi vijavyo.

    Shukran za dhati msikilizaji wetu Amos Msanga kwa barua yako fupi lakini ina ujumbe mzito, kwa kweli suala la mazingira ni gumu sana kwani watu wengi wanasahau kuwa utunzaji wa mazingira ndio unaosababisha hali ya hewa kuwa nzuri, kwa mfano ukikata miti kwa wingi, basi mvua hukosekana, ama kulisha mifugo katika eneo moja kwa muda mrefu kunasababisha jangwa, hivyo ni vyema watu wakawa wanaelimishwa umuhimu wa mazingira kwa binaadamu, ahsante sana.

    Sasa tunawasomea ujumbe wa wasikilizaji wetu kupitia tovuti yetu, kwanzaa ni Seleman baruapepe yake ni sulekazi@yahoo.com anasema leo ujumbe wangu unahusu tamthiliya ya Doudou na mama wakwe zake. Kwani video hii iliacha kuonyeshwa TBC1. Tunaomba irudishwe tuendelee kujifunza utamaduni wa Kichina.

    Gerald Raphael wa Burundi anasema nawapongeza kwa vipindi vyenu ila ningependekeza vipindi vyenu visikike kwa njia ya station za masafa mafupi sw kwani kwa njia ya mw hamuikiki vizuri.

    Suna Omari Mwamkowa baruapepe yake ni omarisuna@yahoo.com anasema naipongeza radio CRI pamoja na watangazaji wote hasa bwana moses ambaye amenifanya niijue lugha ya kichina.

    Abdulla anasema mimi nipo hapa Shenzhen-China. Ningependelea kuzungumza na mtangazaji mmoja wa CRI. Namba yangu ya simu ni 13246797505

    Sam Sabhi baruapepe yake ni samwelsabhi2006@gmail.com, anasema naipenda sana idhaa ya kiswahili China kila la heri!

    Dotto Charles Kajole S.L.P 210 CHATO anasema maoni yangu ni kuhusu tamthiliya ya "Doudou na mama wakwe zake" Niliipenda lakini sikubahatika kuona mwisho wake ulikuwa vipi. Ni vizuri kama mtatoa angalau dvd yake.

    ogutu daniel odhiambo danogu@yahoo.com China bado iko mbele kwa kukuza utamaduni wao. pongezi jamii ya uchina.

    Mwangu 90687 nafurahia sana matangazo yenu

    Nisagurwemmbuji vipindi vyenu vizuri sana tunaomba ushirikiano wenu Tanzania na China uendelee milele

    Nazael Piniel S.L.P 30 Mto wa mbu anasema maoni yangu ni kuhusu tamthia ya Mao Douduo na wakwe zake. Kweli nilipendwezwa sana na tamthilia nampongeza sana Mao Douduo pamoja na waandaaji wote mimi napenda sana kuigiza na ni mpezi wa tamthilia pamoja na nyimbo za kichina na muomba Mao Douduo aandaye tamthilia nyingine nitafurahi sana, pi naomba mnitumie makala ya wiki hii ya kuwa nami jifunze kichina

    Serge baruapepe yake ni sergemuzusangabo@yahoo.fr kutoka east-congo Jamhuri ya kidemokrasi ya kongo, anasema tuna wapata vizuri kidogo kwenye SHOT WAVE huku Kongo ya mashariki nchini Jamhuri ya kidemokrasia Kongo, tunapenda sana vipindi vyenu hasa kile cha tujifunze kichina na salamu zenu. Naomba kwa viongozi wa CRI waimarishe mitambo

    Yohana marwa magaigwa S.L.P 71 Tarime Mara Tanzania anasema maisha ya ughaibuni yanatofautiana na yale ya nyumbani kutokana na tamaduni ya kule ughaibuni. nasema hivyo kwa sababu katika sehemu mbalimbali duniani kuna mambo tofautitofauti kutegemeana na maisha ya wenyeji wa mahali pale, na kumbe maisha ya ughaibuni yana tofauti isipokuwa kinachounganisha watu ni lugha na mahusiano baina ya mtu na mtu, mwisho nawapongeza sana kwa kazi yenu nzuri. Ila ningependa sana tuwasiliane kupitia anwani hii marwa.yohana@yahoo.com ili tuweze kusikiliza CRI vizuri kupitia FM huku DRC.

    Tunawashukuru sana wasikilizaji wetu wote wanaotusikiliza kupitia tovuti yetu, wasikilizaji wengi wanasisitiza kuwa tamthilia ya Doudou na mama wakwe zake ioneshwe tena, kwa mujibu wa makubaliano kati CRI na TBC tamthilia hiyo itaoneshwa tena, hivyo watazamaji wote wenye hamu ya kuiona tena au wale ambao hawakubahatika kuiona hapo kabla wataweza kuiona, ahsante sana.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako