• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • barua 0821

    (GMT+08:00) 2012-08-29 15:34:14
    Barua ya kwanza inatoka kwa msikilizaji wetu Peter Wekesa Yamame wa S.L.P 372 Webuye Kenya, anaanza kwa kusema pokeeni salamu nyingi kutoka kwangu, mimi nina furaha sana kusikiliza mafunzo ya kichina tena kupitia redio ya K.B.C saa nne usiku. Tunaomba mpange siku na mje kututembelea wasikilizaji wenu huku Bungoma magharibi mwa Kenya, tukiwa kama mashabiki wa redio hii. Pia naomba mtutumie fulana, majarida, pia tunataka tuwe na wakala wa habari wa redio China, mwisho tunasema tunawapenda wote watangazaji wa CRI karibuni Bungoma Kenya, ahsante sana.

    Tunakushukuru kwa dhati msikilizaji wetu Peter Wekesa Yamame kwa barua fupi, kuhusu kuja kutembelea huko itakuwa vigumu kidogo kwani hapa idhaa ya Kiswahili tuna pilika nyingi za kuandaa matangazo ya vipindi mbalimbali, lakini kama watangazaji wetu kutoka Kenya wakija likizo, tunaweza kuwaomba watuwakilishe na waje kukutembeleeni huko, hatahivyo kutokuja kukutembeleni haimaanishi kuwa hatupo pamoja nanyi, tunawajali sana wasikilizaji wetu wote, ahsante sana.

    Barua nyingine ni ya Epafra Stanley Deteba wa shule ya sekondari Nanga S.L.P 108 Igunga Tabora, anasema marafiki zangu wapendwa, awali ya yote napenda kuwafahamisha ya kuwa hali ya usikivu wa matangazo yenu ni nzuri kabisa. Februari 4 ya mwaka huu ilikuwa ni siku nzuri sana kwangu, kwani niliweza kufuatilia kwa kina matangazo yenu ambayo yalirushwa hewani kwa uzuri kabisa na katika hali ya umahiri mkubwa sana, niliweza kusikiliza taarifa ya habari, kipindi cha cheche zetu kilichoongelea wasanii kutoka Afrika Mashariki na mwisho niliweza kusikiliza somo la 56 katika kipindi cha kuwa nasi jifunze kichina, kwa ujumla vipindi vyote vilinivutia na kuniongezea maarifa mengi.

    Hongereni CRI kwa kutuandalia vipindi vizuri na ambavyo vinatuelimisha, endeleeni na moyo huohuo, ahsanteni sana.

    Shukrani nyingi sana msikilizaji wetu Epafra Stanley Deteba kwa barua yako, tunapokea pongezi kwa mikono miwili kuhusu uandaaji mzuri wa vipindi, pia tunafurahishwa na ufuatiliaji wako wa matangazo yetu, tunakuomba tu uendelee kusikiliza zaidi matangazo ya vipindi vyetu, na kutoa maoni na mapendekezo yako, ahsante sana.

    Msikilizaji wetu Amos Msanga, mzee wa DW Ludewa Tanzania, baruapepe yake ni amosmsanga@rocketmail.com anasema ni jambo la kusikitisha na kuhuzunisha kuona kuna baadhi ya vijana wa kike wanazaa watoto na kisha kuwatelekeza kiasi kwamba watoto hao hutangatanga mitaani, huwa chokoraa na ombaomba. Kitendo kama hiki ni cha kikatili na ni unyama uliopitiliza. Vijana wa kike na wakiume mnaotenda haya jiangalieni sana, hukumu yenu katika siku ya kiyama itakuwa ni mbaya mtalia na kusaga meno, ni watu gani nyie mnaotupa watoto wenu wakati wanyamapori wanatunza watoto wao. Je, mna maana kwamba ninyi na wanyamapori, wenye akili, utashi, busara na hekima ni wanyama? Kama mnaona Mungu ni adui wenu basi mtiini shetani na fahari zake zote lakini jibu sahihi mtalipata siku ya siku. Ole wenu mnaowatupa watoto.

    Kwanza tunakushukuru sana msikilizaji wetu Amos Msanga kwa maoni yako makali kuhusu vijana wanaozaa watoto na kutelekeza, kwa kweli hili si jambo la kiungwana hata kidogo, kwani matokeo yake ni kuwapa taabu watoto hao, na wengine kama ulivyosema hufikia hata kuwa watoto wa mitaani na ombaomba, hapa tunawaasa vijana wote, kutobeba ujauzito wakiwa bado wadogo, au nje ya ndoa kwani hizo ndio sababu zinazopelekea kutupwa kwa watoto hao ambao hawana hata hatia, ahsante sana.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako