• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Makaburi ya watu wengi waliouawa yagundulika katika eneo la Tana River

    (GMT+08:00) 2012-09-18 20:05:50

    Idadi ya watu waliofariki kutokana na mapigano ya kikabila katika eneo la Tana River nchini Kenya inaweza kuongezeka baada ya makaburi ya watu wengi kugunduliwa katika kijiji cha Ozi ambacho ni makazi ya kabila la Wapokomo.

    Naibu msemaji wa jeshi la polisi la Kenya Charles Owino amethibitisha ripoti hiyo na kuongeza kuwa, polisi wanafuatilia kibali cha mahakama ili kufukua makaburi hayo yaliyochimbwa mita 40 kutoka mto Tana na kufanya uchunguzi zaidi.

    Kwa mujibu wa polisi, washambuliaji, haswa Wapokomo walichukua miili ya watu waliouawa katika mapigano yaliyotokea katika vijiji vya Kilengwani na Reketa, na kuizika katika kijiji cha Ozi ambako mashambulizi hayo yalipangwa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako