• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • barua 0904

    (GMT+08:00) 2012-09-25 15:57:46
    Barua ya kwanza inatoka kwa David Nyongesa wa Shule ya Upili ya Sang'alo S.L.P 1014-50200, Bungoma Kenya, anasema nachukua fursa hii kuishukuru idhaa ya Kiswahili ya CRI kuendelea kutupeperushia matangazo yake kwa lugha ya Kiswahili. Zaidi naipongeza sana kwa kuadhimisha miaka 70 tangu ianzishwe. Mimi kama msikilizaji shabiki wa idhaa ya Kiswahili ya CRI pia najivunia na kusherehekea maadhimisho ya miongo saba tangu kuanzishwa kwake.

    Huku nikiendelea kujivunia kuwa mwana CRI, nina hamu kubwa sana ya kukijua kichina chote, ingawa hivi sasa ninafahamu maneno Fulani katika lugha hiyo lakini shida ni matamshi, kwa hiyo ningependa kama inawezekana Idhaa ya Kiswahili mnitumie CD ambayo ina matamshi ya maneno kadhaa ya kichina, kwasababu nakipenda sana kichina na kipindi cha kuwa nasi jifunze kichina, pia ningependa kujua badhi ya maandishi ya kichina.

    Ninataraji kuwa idhaa ya Kiswahili ya redio China kimataifa itanitimizia haya kwa hiyo ninangoja kwa hamu na ghamu majibu kwani hivi karibuni nina imani kwamba mtanitumia viza ya kuja China kuzuru idhaa hii na hivyo nataka niwasalimie kwa kutumia kichina. Xiexie.

    Tunakushukuru sana msikilizaji wetu David Nyongesa kwa maoni yako, pia inaonekana unakifuatilia sana kichina, hata hivyo ombi lako tumeliwasilisha kwa wahusika na hivi karibuni tu utatumiwa vitabu pamoja na CD za kujifunza Kichina, kwahiyo kaa tayari kujifunza zaidi, ahsante sana.

    Sasa ni zamu ya msikilizaji wetu Amos Msanga wa Ludewa Tanzania baruapepe yake ni amosmsanga@rocketmail.com naye anasema navipongeza vyombo vya habari vyote vya ndani na nje ya Tanzania hasa redio zinazotangaza kwa kiswahili kama redio China kwa kutuhabarisha wananchi na kuchangia ukuaji wa lugha ya kiswahili. Jambo moja nawaomba wamiliki wa vyombo hivyo kutokuogopa chochote kwani hizi ni zama za uwazi na ukweli, MKAPA ALIWAHI KUSEMA.

    Shukran za dhati msikilizaji wetu Amos Msanga kwa barua yako fupi, na kuhusu kutoogopa kusema chochote kwenye matangazo yetu, hilo ni suala ambalo linategemea na sera ya chombo fulani cha habari, sera ya redio China ni kutangaza habari bila ya kuchonganisha baina ya nchi na nchi ama raia wa nchi fulani , ahsante sana.

    Na sasa ni maoni ya wasikilizaji wetu mbalimbali tunaanaanza na Juma Fakih wa S.L.P 1324 Zanzibar anasema ama kwa hakika mnapendeza, leo mimi nataka kuwapongeza kwa vipindi vyenu tuu, kwa mfano jamvi la CRI, Cheche zetu, na kile chengine cha Fadhili na anti yangu Pili Mwinyi, nyie mko juu, halafu kinachonifurahisha zaidi ni kile kipindi cha jifunze kichina, ila tatizo mara nyingi nakikosa, kwani hamuwezi kunitumia japo CD zake maana zile lesson nnazo ila nakosa kupata sauti nikasikia wanavyochanika wachina bwana we wacha, ahsanteni sana, ila kama inawezekana nawaomba mnipatie.

    Shukurani nyingi sana msikilizaji wetu Juma Fakih kwa barua yako, tutajitahidi kukutumia CD ili uweze kujifunza kwa ufanisi Kichina, pia tunakuomba wewe na wasikilizaji wetu wengine muendelee kusikiliza matangazo yetu, ahsante sana.

    Na maoni ya mwisho yanatoka kwa Raim Matonange baruapepe yake ni ematonange@hotmail.com anasema Du tamthilia hiyo inatuvutia lakini mmetutolea uhondo huwo likini nzuri, nataka kusema bravo!!! Kwa Mao Douduo big up.

    Tunakushukuru kwa dhati msikilizaji wetu Raim Matonange kwa maoni yako, ni kweli tamthilia ya Doudou na mama wakwe zake ni nzuri, na kwa vile kuna baadhi ya watazamaji wameleta maoni kwamba irudiwe tena, tunajitahidi kuwasiliana na wenzetu wa TBC ili waioneshe tena, ahsante sana.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako