• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • barua 0911

    (GMT+08:00) 2012-09-25 15:58:42
    Barua ya kwanza inatoka kwa msikilizaji wetu Stephen Magoye Kumalija wa S.L.P 1067 Shinyanga Tanzania, anaanza kwa kusema hamjambo wafanyakazi wa idhaa ya Kiswahili ya redio China kimataifa kutoka hapo Beijing, mimi huku pamoja na club yetu ya Kahama CRI Listerners tuko wazima na tunaendelea kuitegea sikio redio yetu pamoja na kuendelea kufanya mawasiliano ya mara kwa mara kwa njia ya barua.

    Zaidi ya hayo ni dhahiri shahiri kuwa nachukua fursa hii ili kuipongeza serikali ya China na serikali ya Ujerumani kwa kutuma kampuni ya kutengeneza barabara ya Isaka mkoa wa Shinyanga mpaka Lusahunga nkoa wa Kagera. Barabara hiyo ambayo inagharimu shilingi za kitanzania zipatazo bilioni 229, itaziunganisha nchi za Tanzania, Rwanda, Burundi, Uganda pamoja na Congo DRC.

    Hivyo basi nazipongeza sana serikali hizo za China na ujerumani kwa jitihada zake za kujitolea kutoa misaada ya kila aina kwa serikali yetu ya Tanzania. Nikiiomba China iendelee kutoa misaada ya kila aina, ahsante sana.

    Tunakushukuru kwa dhati msikilizaji wetu Stephen Magoye Kumalija kwa barua, kwa kweli China ni nchi inayopenda kuimarisha ushirikiano na nchi za Afrika hasa katika kuzisaidia pale zinapohitaji misaada, ikiwemo kama kujenga barabara na miundombinu mingine, lakini mbali na hayo China na Afrika ni marafiki wa tangu enzi na dahari, ndio maana zinaungana mkono kwa kila hali, tunaomba ushirikiano huu udumu milele.

    Barua nyingine inatoka kwa msikilizaji wetu Daniel Khaoya Ngoya wa S.L.P 1674-50200 Bungoma Kenya, naye anasema nachukua fursa hii kuwashukuru idhaa ya Kiswahili ya redio China kimataifa. Kwa kweli imekuwa ngumu sana kuwasiliana kwani sasa ni muda wa miezi mitatu sijapata waraka kutoka kwenu ama kupokea kadi za salamu, mimi kama kiongozi wa klabu ya "CRI YETU" nimepokea maswali mengi sana kutoka kwa mashabiki wa CRI wakilalamika kuwa wanaipenda idhaa ya CRI lakini hawatumiwi kadi za salamu. Hata hivyo mara kwa mara huwa nawahimiza wasife moyo maana idhaa ya CRI yaweza kuwa inashughulikia mambo makuu ya kutunufaisha sisi kama wana-CRI.

    Lakini mara kwa mara hunifahamisha kuwa wangependa muwe mkiwatumia kadi za salamu ili wasalimiane kwa wingi. Pia wanaomba muwe mkiwapa zawadi. Kuna kanisa moja huku Bungoma lijulikanalo kama Christian Harvest Church, kwa kweli limeweza kutusaidia sana maana wametuunga mkono kwa kusema idhaa ya CRI iendelee mbele maana CRI huongoza na nyingine hufuata nyuma kwa mbali. Kulingana na mchungaji wa kanisa hilo Billy Sande alinihakikishia kuwa ataendelea kuwaongoza washirika kuitegea sikio idhaa ya pekee ya CRI. Kwa niaba ya mashabiki wa Bungoma na Kenya kwa ujumla tunaitakia wakati mwema na muendelee vizuri na kazi yenu. Ahsante sana.

    Shukurani nyingi sana msikilizaji wetu Daniel Khaoya Ngoya kwa barua yako, tumejaribu kuongea na muhusika kujua tatizo ni nini hata kadi hazijafika kwa muda mrefu, na amesema kadi anatuma ila huenda zikawa zimechelewa njiani, maana wakati mwengine njia ya posta inachukua muda mrefu sana, pia tunawashukuru sana kwa kazi yenu njema ya kuitangaza CRI huko Bungoma.

    Barua ya mwisho inatoka kwa Bw. Daudi P. Kikoti wa Jambo Rafiki Salamu Club, S.L.P 11105 Dar Es Salaam Tanzania, anasema hakuna anayependa akutwe na majanga, hata marafiki zetu wa Beijing hamjaomba mkutwe na mafuriko! Nasikitika kwamba mmekutwa na janga hilo la mafuriko, nachukua nafasi hii kuwapa pole na kuwatia moyo kwamba sisi marafiki zetu tumesikitika, lakini kitu kimoja tunawatia moyo kwamba msatahamili na mpige moyo kone! Poleni sana, ninyi mliowapoteza marafiki, jamaa na ndugu zenu! Tunawatakia faraja nyingi daima tupo pamoja.

    Tunakushukuru kwa dhati msikilizaji wetu Daudi P. Kikoti kwa barua yako fupi ya kututia moyo, kwa kweli tumeshapoa ndio mambo ya kilimwengu yalivyo. Hata hivyo tunapenda kuishukuru serikali ya China kwa kuchukua hatua za haraka kuwaokoa na kuwahamisha watu waliothirika. Mwisho tunaomba uendelee kusikiliza idhaa ya Kiswahili ya redio China kimataifa na kutoa maoni na mapendekezo yako, ahsante sana.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako