• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • barua 0918

    (GMT+08:00) 2012-09-25 15:59:13
    Barua ya kwanza inatoka kwa msikilizaji wetu Wambura M. Nyamhanga wa klabu ya wasikilizaji ya Kemogemba SL.P 71 Tarime Mara Tanzania, anaanza kwa kusema ningependa kujongea ndani ya kipindi cha sanduku la barua huku nikitoa shukurani zangu za dhati kwa watangazaji Fadhili Mpunji, Pili Mwinyi mama Chen na wengine wote kwa kuniondolea dukuduku la maswali yangu kupitia kipindi cha China Machoni mwetu cha tarehe 10 Mei mwaka huu, pamoja na kipindi cha sanduku la barua cha tarehe 15, Mei mwakaka 2012.

    Kupitia vipindi hivyo viwili nilifurahi kupata majibu muafaka ya masuali yangu mawili, yaliyohusu kufanana na kuoana kwa wachina, nilipata picha halisi kuhusiana na mila na desturi za wachina kwamba hawaoani na vilevile hawafanani kama nilivyokuwa nafikiria. Hata hivyo utofauti uliopo kidogo ni kati ya wachina wa kaskazini na wale wa kusini, kwani wachina wa kaskazini ni warefu na wanene na wale wa kusini ni wafupi na pia ni wembamba. Nikirejea msemo usemao usilolijua ni sawa na usiku wa kiza, nami niliuliza mkanijibu na sasa nimeondioka kizani. Kila la kheri katika shughuli zenu za kila siku.

    Tunakushuru sana msikilizaji wetu Wambura M. Nyamhanga kwa barua yako ya shukurani, kwa kujibiwa maswali yako yaliyokuwa yakikutatiza kwa muda mrefu, kwa kweli hata sisi pia tunafurahia kuwafahamisha mambo mbalimbali ya hapa China yakiwemo ya utamaduni, mila, desturi, uchumi na mengineyo. Kwani lengo letu hasa ni kuwajuza mambo mbalimbali ya China na ya kote duniani. Kwa hiyo wale wenye mawazo au mitazamo tofauti tunaweza kuwafahamisha kwa undani na hatimaye kuijua China na watu wake, ahsante sana.

    Barua nyingine inatoka kwa msikilizaji wetu Geofrey Wandera wa EVEREADY SECURITY GUARD S.L.P 57333 Nairobi Kenya, naye anasema kwa miaka kadhaa ambayo imepita, na jinsi ambavyo nimeweza kusikiliza na kufuatilia matangazo ya redio China kimataifa, kuna mambo mengi ya ukweli ambayo nimeyapata kuhusu China kinyume na hapo awali.

    Jambo la kwanza, China husema na kutenda huo umekuwa wito wa China siku zote kufuata kiutaratibu maazimio husika ni suala la lazima kwa China, kwa kila aina yoyote ya ushirikiano China huweka alama ya tone lenye kumbukumbu kwa mujibu wa historia yake, kwa hakika chochote mkono wa China ugusapo huwacha alama yenye uthibitisho wa urafiki wa kudumu. Kinachonifurahisha na kuniridhisha ni kwamba dunia nzima kwa sasa inatambua kiukamilifu mshikamano wa kudumu wa China.

    Pamoja na hayo China siku zote hufungua ukurasa mpya wenye azimio la matumaini kwa dunia, kama kuna watu wanaoipenda nchi yao ni wachina na ndio maana hatima ya China huamuliwa na wachina wenyewe bilioni moja nukta tatu, ukweli uliowazi ni kuwa msingi wa China ni nguvu kazi ya watu wake, hata hivyo kulinda na kuendeleza sera na mazungumzo ni mchakato wa siku zote wa China, rasimu ya China inaonesha bayana kuwa, siku zote China hunyanyua bendera yake kwa njia ya amani. Picha ya China inadhihirisha wazi kuwa inapenda kuwakaribisha wageni, kutoka tabaka mbalimbali humu duniani.

    Kila mara huwa napendezwa na kuridhishwa na mifumo inayotolewa na China ambayo huasaidia kukuza na kuinua maendeleo na uchumi kwa haraka. Ingawa kuna mengi ambayo China imeyafikia kihalisi ambayo kwa leo sitayajidili hapa. Pongezi zangu mara dufu ziende kwa CRI kwani kama sio CRI, China isingejulikana vilivyo kama sasa. Pamoja na maendeleo hayo ya China, yangekuwa yanadhoofishwa na vyombo vya habari vingine ambavyo ushawishi wake ni kutoka nchi za magharibi, ahsante sana.

    Shukrani za dhati msikilizaji wetu Geofrey Wandera kwa barua yako, kama ulivyosema, China inajitahidi sana kushirikiana na nchi mbalimbali duniani, na kuweza kusaidia nchi zenye mahitaji ya kusaidiwa hususana marafiki wa Afrika. China pia inapenda kufuata sera yake ya kutoingilia kati mambo ya nchi nyingine, pia China inaamini kwamba ni vizuri hatma ya nchi Fulani ikaamuliwa na nchi hiyo, na ndio maana China inajaribu kutetea nchi yoyote ile duniani ambayo inatendewa mambo ambayo si halali, ahsante sana.

    Sasa ni zamu ya msikilizaji wetu Ramadhan Hamisi wa S.L.P 14-40602 Ndori Kenya, anaanza kwa kutusalimia asalam aleikum, natumai kuwa bado mmesimama kidete mithili ya chuma cha pua, hata baada ya kudidimia kwa uchumi wa dumia mwaka uliopita, kwani bado mnaweza kujiboresha na kujiimarisha zaidi. Huku niliko sote tuko salama na tunazidi kukuombeeni kwa rabuka awajaalie makubwa na kuimarisha maisha yenu. Nawashukuru kwa jarida la daraja la urafiki, mlilonitumia kwani limenijuza mengi kuhusu China.

    Nimepokea salamu za mkuu wa CRI kwa furaha na ninawapa heko kwa matangazo yenu, mmeweza kuelewa jinsi ya kuimarisha uchumi wenu, na tunaomba uchumi wenu usididimie. Ningependa kuwasalimu Bwana Salim Agili wa Jordan na Bwana Mbarouk Msabah. Na nigependa tu kuuliza kama kalenda za mwaka 2012 zipo, kwani sijapata hata moja, kwasababu kalenda zenu huvutia machoni mwetu, natumai mtanitumia moja, na nitawashukuru sana, nawaombea maisha marefu, ahsante sana.

    Shukurani nyingi sana msikilizaji wetu Ramadhan Hamisi kwa barua yako, kwanza tumefurahi kwa kututaarifu kuwa umepata jarida la daraja la urafiki tulilokutumia. Lakini kuhusu kalenda za mwaka 2012 kwa sasa itakuwa vigumu kukutumia kwani mwaka ndio tuaelekea kuumaliza, na hata tukikutumia itachukua muda mferu kukufikia, hivyo tungeomba ustahamili hadi tutakapotoa kalenda za mwaka 2013. ahsante sana.

    Na sasa tunawasomea ujumbe kutoka kwa wasikilizaji wetu wanaotembelea tovuti yetu, msikilizaji wetu Xavier L. Telly-Wambwa wa S.L.P 1993-50200, Bungoma, Kenya anasema ni vyema sana kumjua huyu mwandishi na hebu Mola azidi kumbariki kwa usikivu wake wa CRI. Asante.

    Tunakushukuru kwa dhati msikilizaji wetu Xavier L. Telly-Wambwa kwa maoni yako mafupi, na kukujibu ni kwamba ungemtaja huyo mwandishi uliyemkusudia kwani kwa kufanya hivyo tungeweza kufisha ujumbe huu kwake, hata hivyo tunapokea dua zako, ahsante sana.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako