• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Japan inapaswa kusahihisha makosa yake kwa vitendo halisi

    (GMT+08:00) 2012-09-25 16:55:52

    Naibu waziri wa mambo ya nje wa China Bw. Zhang Zhijun, leo tarehe 25 amekutana na naibu waziri wa mambo ya nje wa Japan Chikao Kawai hapa Beijing,ambapo wamezungumza kuhusu suala la Visiwa vya Diaoyu. Zhang Zhijun amesema kuwa, China kamwe haitavumilia vitendo vya upande mmoja wa Japan vya kuharibu mamlaka ya ardhi ya China, hivyo Japan inapaswa kujikosoa kwa kina na kusahihisha makosa yake kwa vitendo halisi. Aidha, amesema Japan inatakiwa kurejea katika maoni ya pamoja na maelewano yaliyofikiwa na viongozi wa nchi hizo mbili, na kuchukua hatua pamoja na China ili uhusiano kati ya nchi hizi mbili urudi kwenye njia sahihi ya kuendelea vizuri kwa utulivu.

    Zhang Zhijun amesema, Visiwa vya Diaoyu na visiwa vingine vilivyoko pembezoni mwake viko kwenye ardhi ya China tangu enzi na dahari, na huu ni ukweli wa mambo usiopingika.

    Pande hizo mbili zimekubali kuendelea na majadiliano kuhusu suala hilo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako