• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa Iran asema kuwa Iran inatishiwa na nchi zenye umwamba

    (GMT+08:00) 2012-09-27 18:13:25

    Rais Mahmoud Ahmad-Nejad wa Iran amesema kuwa, nchi yake inatishiwa na "nchi zenye umwamba", hasa imetishiwa na Israel ambayo inataka kufanya mapigano ya kijeshi dhidi yake. Rais Ahmadi-Nejad amesema hayo jana tarehe 26 wakati wa mjadala wa kawaida wa Baraza kuu la 67 la Umoja wa Mataifa.

    Rais Ahmadi-Nejad amesema, mashindano ya silaha ya nchi zenye umwamba na tishio la kutumia silaha za nyuklia na silaha kali vimeongezeka zaidi. Pia amesema kuwa, Israel inaitishia Iran mara kwa mara kwamba itachukua vitendo vya kijeshi dhidi yake, huu ni "mfano halisi katika hali ilivyo ya sasa..

    Katika hotuba iliyotolewa na Rais Barack Obama wa Marekani jumanne katika mkutano huo, rais Obama alisema, anapenda kutatua suala la nyuklia la Iran kwa mbinu ya kidiplomasia, lakini muda ni wenye ukomo. Ameonya kuwa, Iran, ambayo ina silaha za nyuklia, inatishia usalama wa Israel na nchi za ghuba na utulivu wa uchumi wa dunia, na Marekani itachukua hatua za lazima ili kuzuia Tehran kupata silaha za nyuklia. Hatua hiyo itasaidia kuzuia kutokea kwa mashindano ya silaha za nyuklia katika sehemu ya mashariki ya kati, na kuzuia kuharibu Mkataba wa kutoeneza silaha za nyuklia.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako