• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mkutano mkuu wa kamati kuu ya 17 ya Chama cha Kikomunisti cha China kufanyika tarehe 8 Novemba mjini Beijing

    (GMT+08:00) 2012-09-28 19:56:13

    Ofisi ya siasa ya Kamati kuu ya chama cha kikomunisti cha China imeitisha mkutano leo tarehe 28 na kuamua kuwa, Mkutano wa 7 wa wajumbe wote wa Kamati kuu ya 17 ya Chama cha kikomunisti cha China utafanyika tarehe 1 Novemba hapa Beijing. Na ofisi ya siasa ya kamati kuu ya chama itapendekeza Mkutano mkuu wa wajumbe wote wa Kamati kuu ya 18 ya Chama cha kikomunisti cha China ufanyike tarehe 8 Novemba.

    Mkutano wa leo umesisitiza kuwa, mkutano mkuu wa Kamati kuu ya 18 utakuwa ni mkutano muhimu sana, utaangalia kwa makini kazi zilizofanyika na uzoefu uliopatikana katika miaka mitano iliyiopita, utafuata mwelekeo wa maendeleo ya dunia na ya China kwa hivi sasa, kuzingatia kwa pande zote matakwa mapya kuhusu maendeleo ya China na matarajio mapya ya wananchi wa makabila yote, na kutunga kwa njia ya kisayansi mpango wa vitendo na sera na hatua zinazofuata matakwa na matarajio hayo mapya. Mkutano huo pia utaandaa mipango ya kimkakati kuhusu mchakato wa mageuzi na kufungua mlango pamoja na ujenzi wa mambo ya kisasa ya chama, kuendelea kusukuma mbele kazi ya kujiendeleza kwa njia ya kisayansi, kuhimiza masikilizano ya jamii, kuboresha zaidi maisha ya wananchi, na kufanya juhudi zaidi ili kujenga jamii yenye maisha bora kwa pande zote.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako