• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Balozi wa Nigeria nchini China asema mkutano wa 18 wa CPC utahimiza uhusiano kati ya China na Afrika

    (GMT+08:00) 2012-10-17 17:29:49

    Balozi wa Nigeria nchini China Aminu Bashir Wali, leo hapa Beijing amesema, mkutano mkuu wa Kamati kuu ya 18 ya Chama cha Kikomunisti cha China utakaofanyika hivi karibuni hakika utasukuma mbele maendeleo ya China na uhusiano kati ya China na Afrika.

    Balozi Wali amesema, katika zaidi ya miaka 60 iliyopita, China imepata maendeleo makubwa, na nchi nyingi zimefikia kiwango hicho cha maendeleo kwa miaka mia 2 au 3. Amesema wananchi wa China, chini ya uongozi wa Chama cha Kikomunisti cha China, wanatilia maanani kujifunza uzoefu wa kihistoria, kwani hiki ni Chama kinachojitahidi kujifunza.

    Balozi Wali amesema, chini ya uongozi wa Chama hicho, serikali ya China imefanya juhudi kubwa katika kuendeleza ushirikiano wa kiwenzi na nchi za Afrika, na kuzisaidia nchi hizo kutatua matatizo mbalimbali. Amesema jambo hilo linajulikana duniani, pia ni maoni ya pamoja ya mabalozi wa nchi mbalimbali nchini China.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako