Mlibya anayetuhumiwa na Misri kwa kuhusika katika shambulizi dhidi ya ubalozi wa Marekani nchini Libya mwezi uliopita ameuawa baada ya jeshi la usalama la Misri kuvamia sehemu moja huko Cairo. Ofisa wa usalama wa Misri amesema mlibya huyo aliuawa kwenye operesheni iliyomlengea yeye na wapiganaji wengine wanaotuhumiwa kuwa na uhusiano na kundi la Al-Qaeda. Wamisri wanne pia walikamatwa kwenye opresheni hiyo. Mlibya huyo aliyetambuliwa kwa jina la Karim Ahmed Essam el-Azizi, aliuawa kwa bomu alilokuwa akijaribu kulipua walipovamiwa. Watu wanaoishi karibu na sehemu hiyo walisema operesheni hiyo ilikuwa kali sana.
(sauti)
"Nilikuwa niko katikati, na risasi zilikuwa zikitoka pande zote, kushoto na kulia. Jengo linalowaka moto lilikuwa kushoto kwangu, na lililokuwa mbele yangu lilikuwa likiwaka, mimi nilizingirwa."
Shambulizi dhidi ya ubalozi wa Marekani nchini Libya lilisababisha kifo cha balozi na maofisa wengine watatu wa Marekani. Rais wa Marekani na maofisa wengine wa nchi hiyo wamesema shambulizi lilikuwa ni kitendo cha kigaidi kilichofanywa na wapiganaji wenye uhusiano na kundi la Al Qaeda.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |