Kampuni kubwa kabisa ya kuchimba madini ya platinum ya Anglo-American ya Afrika Kusini imefanya mazungumzo na vyama vya Wafanyakazi na wajumbe wa wafanyakazi tangu tarehe 26 mwezi huu, na kufikia makubaliano kuwa wafanyakazi elfu 12 waliofukuzwa kazi kutokana na mgomo watarudishwa kazini kama watatekeleza agizo la kurudi kazini kabla ya tarehe 30. Makubaliano hayo yanatazamiwa kumaliza mgomo uliodumu kwa miezi 6 na kusababisha hasara ya zaidi ya Rand bilioni 11 za Afrika Kusini, kusababisha mitaji mingi kwenda nje ya nchi hiyo, na kushuka kwa thamani ya Rand ya Afrika Kusini ambayo imefikia kiwango cha chini kabisa katika miaka 3 na nusu iliyopita.
Msemaji wa shirikisho la Wafanyakazi la Afrika Kusini alisema, kampuni hiyo imeahidi kuendelea na mazungumzo na vyama vya Wafanyakazi na ofisa wa idara ya madini kuhusu mishahara ya wafanyakazi.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |