• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Ongezeko la mwaka la uwekezaji wa serikali ya China katika mambo ya kilimo, vijiji na wakulima lafikia asilimia 21 katika miaka 10 iliyopita.

    (GMT+08:00) 2012-10-30 16:05:12

    Wizara ya fedha ya China imesema, kuanzia mwaka 2003 hadi mwaka huu, fedha zilizotolewa na serikali kuu ya China katika mambo ya kilimo, vijiji na wakulima zimefikia zaidi ya yuan trilioni 6, ongezeko lake la mwaka limefikia asilimia 21.

    China ikiwa nchi kubwa inayotegemea zaidi kilimo, tangu mkutano mkuu wa 16 wa Chama cha Kikomunisti cha China ufanyike mwaka 2002, serikali iliamua kutoa kipaumbele katika mambo ya kilimo, vijiji na wakulima. Katika kutekeleza hayo, serikali kuu kwanza iliamua kuongeza aina za ruzuku kwa kilimo, vijiji na wakulima na kupanua maeneo yake, na hadi kufikia mwaka huu, ruzuku hizo zimefikia yuan bilioni 200. Pili, serikali kuu imeendelea kutenga zaidi fedha, kukamilisha sera na na hatua husika, na kutilia mkazo zaidi ujenzi wa miundo mbinu ya vijijini. Aidha, serikali kuu imeongeza kwa kiasi kikubwa matumizi kwa ajili ya maendeleo ya mambo ya jamii vijijini. Hadi mwaka 2012, matumizi hayo yamefikia nusu ya matumizi yote katika mambo ya kilimo,vijiji na wakulima.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako