• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Vyama vya kisiasa barani Afrika vyautakia mafanikio mkutano mkuu wa 18 wa Chama cha Kikomunisti cha China

    (GMT+08:00) 2012-11-02 17:47:16

    Vyama vingi vya kisiasa barani Afrika vimeutakia mafanikio makubwa Mkutano mkuu wa 18 wa Chama cha Kikomunisti cha China ambao utafanyika hivi karibuni. Pia vimeeleza matumaini ya kuimarisha mawasiliano kati yao na Chama cha Kikomunisti cha China.

    Naibu mkurugenzi wa Idara ya mawasiliano na nje ya kamati kuu ya Chama cha kikomunisti cha China inayoshughulika na masuala ya kusini mwa Afrika, Jia Chen, leo alipohojiwa na mwandishi wa habari wa CRI amesema, vyama vya kisiasa barani Afrika vinafuatilia sana mkutano huo utakaofanyika hivi karibuni, na vimetuma salamu za kuutakia mkutano huo mafanikio. Amesema vyama vya kisiasa barani Afrika vinatilia maanani urafiki kati yao na Chama cha Kikomunisti cha China, pia vinakishukuru Chama hicho kwa mchango wake katika mchakato wa uhuru wa Afrika.

    Habari nyingine zinasema, mwenyekiti wa chama tawala cha PDP nchini Nigeria, Bamanga Tukur, jana amesema, mkutano mkuu wa 18 wa Chama cha Kikomunisti cha China utakaofanyika hivi karibuni ni msingi mpya wa maendeleo ya China, na anavitaka vyama hivyo viwili viimarishe mawasiliano na kujifunzana uzoefu wa utawala.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako