• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mkutano wa saba wa wajumbe wote wa kamati kuu ya 17 ya Chama cha Kikomunisti cha China wafungwa hapa Beijing

    (GMT+08:00) 2012-11-04 20:17:05

    Mkutano wa saba wa wajumbe wote wa kamati kuu ya 17 ya Chama cha Kikomunisti cha China ulioanza tarehe 1 umemalizika leo hapa Beijing. Katibu mkuu wa kamati kuu ya chama Bw. Hu Jintao ambaye pia ni rais wa China ametoa hotuba muhimu kwenye mkutano huo ulioendeshwa na ofisi ya siasa ya kamati kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China. Mkutano huo umeamua kuwa mkutano wa 18 wa wajumbe wote wa Chama cha Kikomunisti cha China utaanza tarehe 8 mwezi huu mjini Beijing.

    Mkutano huo ulisikiliza na kujadili ripoti iliyotolewa na Bw. Hu Jintao kwa kufuata maagizo ya ofisi ya siasa ya kamati kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China. Aidha mkutano huo pia ulipitisha ripoti iliyotolewa na kamati kuu ya 17 ya chama kwa mkutano mkuu wa 18 wa chama, na mswada wa marerekebisho ya Katiba ya Chama cha Kikomunisti cha China, na kuamua kuwasilisha nyaraka hizo mbili kwa mkutano mkuu wa 18 wa Chama cha Kikomunisti cha China.

    Mkutano huo pia ulichambua hali na majukumu ya hivi sasa, na kujadili masuala muhimu kadha wa kadha ya kuendeleza mambo ya ujamaa wenye umaalum wa China, na ujenzi wa Chama cha Kikomunisti cha China, ili kufanya maandalizi kwa ajili ya kufanyika kwa mkutano mkuu wa 18 wa chama cha kikomunisti cha China.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako