• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Vyombo vya habari vya lugha ya Kichina nchini Marekani vyafuatilia sana mkutano mkuu wa 18 wa Chama cha kikomunisti cha China

    (GMT+08:00) 2012-11-06 10:33:29

    Mkutano mkuu wa 18 wa Chama cha Kikomunisti cha China unakaribia, na vyombo vya habari vya lugha ya Kichina nchini Marekani vinafuatilia sana mkutano huo, na vimejitahidi kuuripoti na kuueleza kwa pande zote na kwenye ngazi mbalimbali. Vyombo hivyo vimesema kuwa mkutano huo utafungua ukurasa mpya wa maendeleo ya China.

    Makala iliyotolewa na gazeti la The China Press imesema tangu utekelezaji wa sera ya mageuzi na ufunguaji mlango uanze, kila baada ya mkutano mkuu wa Chama cha kikomunisti cha China kufanyika, chama hicho huweza kupata maendeleo makubwa katika uvumbuzi wa nadharia, halafu kuchukua hatua mara moja kutekeleza nadharia hiyo.

    Siku hizi tovuti ya SinoVision Net ya Marekani imetoa ripoti kuwa mkutano mkuu wa 18 wa Chama cha kikomunisti cha China utakuwa mnara mpya katika mambo ya siasa nchini China. Aidha, mkutano huo utaonesha ishara yenye nguvu, kwamba katika hali ya msukosuko wa kiuchumi kote duniani, Chama cha kikomunisti cha China kina mshikamano wa ndani unaohitajika katika kufanikisha kazi ya kushughulikia mambo ya umma na kusukuma mbele ongezeko endelevu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako