• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Maandalizi ya Mkutano mkuu wa 18 wa Chama cha Kikomunisti cha China yakamilika

    (GMT+08:00) 2012-11-07 21:32:36

    Mkutano mkuu wa 18 wa Chama cha Kikomunisti cha China unatarajiwa kufunguliwa kesho tarehe 8 hapa Beijing. Kwenye mkutano na waandishi wa habari uliofanyika leo, msemaji wa mkutano huo Bw. Cai Mingzhao amefahamisha hali husika kuhusu mkutano huo, pia amejibu maswali yaliyotolewa na waandishi wa habari kuhusu kazi za kuboresha maisha ya wananchi, kupambana na ufisadi na kufanya mageuzi ya mfumo wa kisiasa.

    Msemaji huyo amesema, Mkutano huo utajulisha kwa makini kazi zilizofanyika katika miaka mitano iliyopita na uzoefu wa chama tokea mkutano mkuu wa 16 wa chama; utatunga mpango wa utekelezaji kwa njia ya kisayansi ambao utaambatana na matakwa ya zama za hivi sasa na matumaini ya wananchi, na kupanga mpango wa kimkakati kwa ajili ya kusukuma mbele mageuzi na ufunguaji mlango na ujenzi wa mambo ya kisasa ya ujamaa, pamoja na kuhimiza kwa pande zote mradi mpya mkubwa wa ujenzi wa chama".

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako