• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mkutano mkuu wa 18 wa CPC wafunguliwa

    (GMT+08:00) 2012-11-08 09:46:01

    Mkutano mkuu wa 18 wa Chama cha Kikomunisti cha China CPC umefunguliwa leo asubuhi hapa Beijing, viongozi wa juu na wajumbe 2,300 wa chama hicho wanahudhuria mkutano huo. Katibu mkuu wa chama hicho Bw. Hu Jintao ametoa ripoti ya utendaji kwenye mkutano mkuu huo kwa niaba ya kamati kuu ya awamu ya 17, ripoti hiyo itapitiwa na wajumbe wote. Kwenye ripoti hiyo, Chama cha Kikomunisti cha China kinasema kitaendelea kuongoza nchini kwa kufuata njia ya ujamaa wenye umaalumu wa China.

    Ajenda ya mkutano huo inaonesha kuwa, katika siku 7 zijazo wajumbe watapitia ripoti iliyotolewa na Bw. Hu Jintao, kujadili na kupitisha rasimu ya marekebisho ya Katiba ya Chama cha Kikomunisti cha China, kupitia ripoti ya kazi iliyotolewa na kamati ya nidhamu ya kamati kuu ya chama hicho, na kufanya uchaguzi wa wajumbe wa kamati kuu ya awamu mpya ya Chama cha Kikomunisti cha China na kamati mpya ya nidhamu ya chama hicho.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako