• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Viongozi wa nchi za nje waona mkutano mkuu wa 18 wa Chama cha Kikomunisti cha China utaathiri mambo ya dunia

    (GMT+08:00) 2012-11-08 16:13:18

    Mkutano mkuu wa 18 wa Chama cha Kikomunisti cha China umefunguliwa leo tarehe 8 asubuhi hapa Beijing. Viongozi wengi wa nchi za nje wanafuatilia sana mkutano huo na kusifu mafanikio makubwa yaliyopatikana nchini China katika miaka 10 iliyopita, na wanaona kuwa mkutano huo utaathiri mambo ya uchumi na siasa ya dunia.

    Mwenyekiti wa Chama tawala nchini Sri Lanka, Maitripala Sirisena ametuma salamu za pongezi na kuutakia mafanikio mkutano huo ulioanza rasmi leo.

    Naye naibu waziri wa mambo ya nje wa Bosnia Herzegovina, Amer Kapetanovic amesema, mkutano huo utaendeleza urafiki na ushirikiano wa jadi baina ya nchi hizo mbili, na China itaonesha umuhimu wake zaidi kwa maendeleo ya dunia katika miaka 10 ijayo.

    Waziri wa mambo ya nje wa Nepal, Narayan Kaji Shrestha amesema, anaamini kwamba baada ya mkutano huo, Chama cha Kikomunisti cha China kitawaongoza wananchi wa China katika kuijenga nchi yao iwe na usitawi na neema zaidi.

    Na Naibu Spika wa bunge la Vietnam, Uong Chu Luu amesema, mkutano huo ni tukio muhimu kwa China na wananchi wake, hata wananchi wa Vietnam wanatarajia mkutano huo kufanyika na kupata mafanikio.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako