• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mapato ya serikali ya China yaongezeka kwa asilimia 20.82 kwa mwaka

    (GMT+08:00) 2012-11-09 17:50:32

    Wizara ya fedha ya China imesema, mapato ya serikali ya China yameongezeka kutoka yuan trilioni 1.89 za mwaka 2002 hadi yuan trilioni 10.37 katika mwaka 2011, na hili ni ongezeko la asilimia 20.82 kwa mwaka.

    Makala iliyotolewa jana kwenye tovuti ya wizara hiyo imesema, katika miaka kumi iliyopita, China imekuwa ikifanya mageuzi katika mambo ya fedha, kujenga na kukamilisha utaratibu wa kudumisha ongezeko lenye utulivu la mapato ya serikali, hatua ambayo imehimiza mapato ya serikali kuongezeka mwaka hadi mwaka. Takwimu zimeonesha kuwa, matumizi ya fedha ya serikali yameongezeka kuanzia trilioni 2.21 mwaka 2002 hadi yuan trilioni 10.89 mwaka 2011, hili ni ongezeko la asilimia 19.39 kwa mwaka. Wakati huo huo, muundo wa matumizi ya fedha pia umezidi kuboreshwa, fedha zinazotumiwa katika mambo ya utoaji huduma kwa umma kama vile ya elimu, matibabu na afya, huduma za jamii na utoaji wa nafasi za ajira zimekuwa zikiongezeka kwa hatua madhubuti.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako