• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Viongozi wa China washiriki katika majadiliano na wajumbe kutoka mikoa mbalimbali wanaohudhuria mkutano mkuu wa 18 wa CPC

    (GMT+08:00) 2012-11-09 18:32:57

    Mkutano mkuu wa 18 wa Chama cha Kikomunisti cha China umefunguliwa jana alasiri hapa Beijing. Rais Hu Jintao wa China leo ameshiriki kwenye majadilino na wajumbe kutoka mkoa wa Jiangsu na kudhihirisha kuwa, ripoti iliyotolewa jana kwenye mkutano huo ni taarifa ya kisiasa na mpango wa utekelezaji wa Chama cha Kikomunisti cha China kwa ajili ya kujipatia ushindi mpya katika ujenzi wa ujamaa wenye umaalum wa China. Amesema chama hicho kinapaswa kuchukua muda wa kujifunza na kutekeleza ripoti hiyo kama mwanzo mpya, kufahamu vizuri majukumu, kuendelea kushikamana na kufanya kazi kwa bidii, ili kupata mafanikio makubwa zaidi.

    Viongozi wengine wa China akiwemo spika wa bunge la umma la China Wu Bangguo, waziri mkuu Wen Jiabao na mwenyekiti wa baraza la mashauriano ya kisiasa la China Jia Qinglin jana alasiri pia walishiriki kwenye mijadala ya wajumbe kutoka sehemu mbalimbali nchini China wanaohudhuria mkutano mkuu wa 18 wa Chama cha Kikomunisti cha China.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako