• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Viongozi wa nchi mbalimbali duniani waupongeza mkutano mkuu wa 18 wa CPC

    (GMT+08:00) 2012-11-09 19:51:43

    Viongozi wa nchi mbalimbali duniani wametoa salamu za pongezi kwa Mkutano mkuu wa 18 wa Chama cha Kikomunisti cha China unaoendelea hapa Beijing..

    Rais Omar al-Bashir wa Sudan amesema mkutano huo ni muhimu sana, kwani unalenga kuboresha maisha ya wananchi wa China. Aidha, wakati dunia inakabiliwa na mabadiliko makubwa, nchi ya China, na Chama cha Kikomunisti cha China, vinafanya kazi muhimu katika kukabiliana na mabadiliko hayo.

    Rais Michael Sata wa Zambia amesema, mkutano huo ni kwa ajili ya kupanga mustakabali wa China, na anaamini kuwa mkutano huo utapata mafanikio.

    Waziri mkuu wa Uganda Amama Mbabazi amesema, wananchi wa China wanasonga mbele kwa kufuata njia ya ujenzi wa mambo ya kisasa ya ujamaa chini ya uongozi wa Chama cha Kikomunisti cha China.

    Naye katibu mkuu wa Chama cha ukombozi wa umma cha Sudan Kusini amesema, maamuzi ya mkutano huo mkuu utaijenga China kuwa nchi inayostawi, na kutoa mchango mkubwa kwa ajili ya amani na ustawi wa binadamu wote.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako