• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Njia inayofuata China yasifiwa

    (GMT+08:00) 2012-11-11 19:59:37

    Wakati mkutano mkuu wa 18 wa chama cha kikomunisti cha China CPC unapoendelea hapa Beiijing, watu kutoka nchi mbalimbali wanasema mafanikio makubwa ya China yametokana na njia ya maendeleo iliyofuata katika kipindi cha miaka 10 iliyopita.

    Mkurugenzi wa taasisi ya utafiti wa maliasili wa kusini mwa Afrika Bw. Kabenba amesifu njia inayofuatwa na China akisema ni mfano wa kuigwa na nchi za Afrika kwa kuwa ndiyo chanzo cha nguvu ya China na kuwawezesha wananchi wake.

    Naibu kiongozi wa chama cha uhuru cha Australia Bw. Bishop amesema, China inashikilia kujiendeleza kwa njia ya amani, kuwaondolea umaskini mamilioni ya watu, akisema hayo ni mafanikio ambayo hayajawahi kuonekana katika historia ya binadamu.

    Pierre Pical ambaye ni Daktari wa sayansi ya geopolitics kutoka Ufaransa anaona kuwa China imeiletea dunia njia mpya ya maendeleo, ambayo ni ya amani zaidi na yenye kuhimiza masikilizano.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako