• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yaendelea kuhamasisha watu binafsi kuwekeza katika shughuli za benki

    (GMT+08:00) 2012-11-12 18:29:07

    Mjumbe wa mkutano mkuu wa 18 wa Chama cha Kikomunisti cha China ambaye pia ni mwenyekiti wa kamati ya usimamizi wa benki za China Shang Fulin amesema, China itaendelea kuhamasisha watu binafsi kuwekeza katika shughuli za benki.

    Shang amesisitiza kuwa China inaweka vigezo, vidhibiti na masharti ya ya pamoja kwa mitaji ya aina mbalimbali kuingia katika shughuli za Benki au shughuli nyingine. Mwezi Mei mwaka huu kamati hiyo ilitoa waraka wa utekelezaji kuhusu kuwahamasisha watu binafsi kuwekeza katika shughuli za benki nchini China, kuunga mkono mitaji ya watu binafsi na mitaji mingine kuingia shughuli hizo kwa masharti sawa, na kujenga mazingira mazuri kwa wawekezaji binafsi.

    Bw. Shang amesema, hadi kufikia mwishoni mwa mwaka jana, mitaji ya watu binafsi imechukua asilimia 50 katika benki ndogo na za ukubwa wa kati za kibiashara nchini China. Na katika benki kama hizo vijijini, mitaji ya watu binafsi imechukua asilimia 90.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako