• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China kushikilia kanuni ya "Ushirikiano na maendeleo kwa pamoja" katika mambo ya diplomasia

    (GMT+08:00) 2012-11-12 19:58:17

    Mkutano mkuu wa 18 wa Chama cha Kikomunisti cha China unaoendelea hapa Beijing umefafanua sera zake kuhusu mambo ya ndani na mambo ya diplomasia. Ufafanuzi huo umetolewa kwenye ripoti yake iliyowasilishwa kwenye mkutano huo.

    Ripoti hiyo inasema, China itajitahidi kuyafanya maendeleo yake yazinufaishe pia nchi jirani zake. Mtafiti wa taasisi ya mambo ya kimataifa na kimkakati Gao Zugui anaona kuwa, ushirikiano wa kunufaishana ulioendelea kwa miaka mingi kati ya China na nchi jirani umeifanya China iwe mwenzi mkubwa zaidi wa biashara kwa nchi nyingi jirani ikiwemo Japan, na katika siku za baadaye, China itaendelea kuhimiza ushirikiano kati ya nchi za kikanda ili kupata maendeleo kwa pamoja.

    Kuhusu migongano ya haki na maslahi ya ardhi na bahari kati ya China na baadhi ya nchi jirani iliyoibuka hivi karibuni, naibu mkuu wa Chuo kikuu cha Mambo ya Kidiplomasia cha China Qin Yaqing anaona kuwa, ripoti hiyo imesisitiza kulinda haki na maslahi kwenye bahari, hii ni muhimu sana, kwani nchi yoyote yenye mamlaka inapaswa kufanya hivyo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako