• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wajumbe wa kudumu wa Ofisi ya siasa ya Kamati kuu ya 18 ya Chama cha Kikomunisti cha China wakutana na waandishi wa habari

    (GMT+08:00) 2012-11-15 15:05:27

    Katibu mkuu mpya wa Kamati kuu ya 18 ya Chama cha Kikomunisti cha China Xi Jinping na wajumbe wengine wa kudumu wa Ofisi ya siasa ya Kamati kuu ya chama hicho Li Keqiang, Zhang Dejiang, Yu Zhengsheng, Liu Yunshan, Wang Qishan na Zhang Gaoli waliochaguliwa kwenye mkutano wa kwanza wa wajumbe wote wa Kamati kuu ya 18 ya chama hicho, wamekutana na waandishi wa habari wa nchini na wa nje leo tarehe 15 asubuhi katika Jumba la mikutano ya umma la Beijing.

    Kwenye mkutano huo, Xi Jiping amedhihirisha kuwa, jukumu letu ni kuwa na mshikamano na kuwaongoza wanachama wote na wananchi wa makabila yote katika kuendelea kupigania kwa juhudi lengo la kusitawisha taifa la China; kuendelea kujikomboa kifikra, kushikilia mageuzi na ufunguaji mlango, kukuza tija ya uzalishaji kwenye jamii, kujitahidi kuondoa taabu zinazowakumba umati wa watu katika uzalishaji na maisha, na kufuata kithabiti njia ya kujiendeleza kwa pamoja. Jukumu letu pia ni kujiunga na wanachama wote katika kushughulikia kwa makini matatizo yaliyopo ndani ya chama, kurekebisha mtindo wa kazi, kuwasiliana kwa karibu na umati wa watu, ili chama chetu siku zote kiwe kiini cha uongozi imara wa mambo ya ujamaa wenye umaalumu wa China.

    Xi Jinping ameongeza kuwa, China inahitaji kuielewa zaidi dunia, dunia pia inahitaji kuielewa zaidi China. Ametumaini kuwa waandishi wa habari na marafiki wataendelea na juhudi na kutoa mchango kwa ajili ya kuongeza maelewano kati ya China na nchi mbalimbali duniani.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako