• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Viongozi wapya wa Kamati kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China wajitokeza

    (GMT+08:00) 2012-11-15 18:48:30

    Leo tarehe 15, mkutano wa kwanza wa wajumbe wote wa Kamati kuu ya 18 ya Chama cha Kikomunisti cha China umefanyika hapa Beijing. Baada ya mkutano huo, katibu mkuu mpya wa Kamati kuu ya chama hicho Bw. Xi Jinping aliongoza wajumbe wapya wa kudumu wa ofisi ya siasa ya kamati kuu ya chama Bw Li Keqiang, Bw Zhang Dejiang, Bw Yu Zhengsheng, Bw Liu Yunshan, Bw Wang Qishan na Bw Zhang Gaoli kukutana na waandishi wa habari wa nchini na nje. Katika hotuba yake kwenye mkutano huo, Xi Jinping alisema:

    "Jukumu letu ni kuwa na mshikamano na kuwaongoza wanachama wote na wananchi wa makabila yote katika kuendelea kupigania kwa juhudi lengo la kusitawisha taifa la China;

    Jukumu letu pia ni kujiunga na wanachama wote katika kushughulikia kwa makini matatizo yaliyopo ndani ya chama;

    Jukumu letu ni kujitahidi kuondoa taabu zinazoukumba umma katika uzalishaji na maisha, na kufuata kithabiti njia ya kujiendeleza kwa pamoja…"

    Hotuba ya Xi Jinping imeonesha kuwa viongozi wapya wa kamati kuu ya chama wanatilia maanani mambo ya umma. Amesisitiza kuwa, wananchi wa China ni wananchi waostahili kusifiwa, matarajio ya wananchi ndio malengo wanayopaswa kupigania viongozi wa chama. Akisema:

    "Wananchi wetu wanapenda maisha, na kutarajia kuwa na elimu bora zaidi, kazi tulivu zaidi, mapato ya kuridhisha zaidi, huduma za jamii za kutegemeka zaidi, huduma za matibabu na afya za kiwango cha juu zaidi, makazi yenye hali nzuri zaidi, na mazingira mazuri zaidi; pia wanatarajia watoto wao waweze kukua vizuri zaidi, kupata ajira nzuri zaidi na kuishi maisha mazuri zaidi. Matarajio ya wananchi juu ya maisha bora ndiyo malengo tunayotakiwa kupigania."

    Katibu mkuu mpya Xi Jinping kwa niaba ya viongozi wapya wengine ameeleza dhamira ya kuendelea na mageuzi na ufunguaji mlango. Amesisitiza kuwa, ni lazima kuendelea kujikomboa kifikra, na kukuza siku hadi siku tija ya uzalishaji kwenye jamii. Kwa mujibu wa maoni ya watu, maneno aliyosema Bw Xi yameonesha nia imara ya viongozi wapya wa kamati kuu ya chama ya kusukuma mbele mageuzi na ufunguaji mlango.

    Kutokana na malengo yaliyothibitishwa kwenye mkutano mkuu wa 18 wa Chama cha kikomunisti cha China, chama hicho kitawaongoza wananchi wa China kukamilisha kazi ya ujenzi wa jamii yenye maisha bora kote nchini ifikapo mwaka 2020, na kutimiza lengo la kuongeza mara dufu mapato ya kila mkazi nchini China. Kuhusu hayo, profesa Xie Chunhui wa Chuo cha kamati kuu ya chama amedhihirisha kuwa, viongozi wapya wa kamati kuu ya Chama cha kikomunisti cha China wanakabiliwa na changamoto nyingi katika kutimiza malengo hayo, na changamoto kubwa zaidi ni kuhusu ujenzi wa chama chenyewe. Kwa mfano ufisadi wa makada fulani ndani ya chama.

    Kuhusu suala la ufisadi, katika hotuba yake ya leo, Xi Jinping amesema, katika hali mpya chama kinakabiliwa na changamoto nyingi kubwa, na ndani ya chama kuna matatizo mengi yanayotakiwa kutatuliwa haraka, hasa matatizo kuhusu ufisadi, kutowasiliana na umma, kurudia mambo yaleyale wakati wa utekelezaji, na kufanya utawala msonge, ni lazima kutoa nguvu kubwa kuyatatua matatizo hayo, na wanachama wote wanapaswa kuwa macho na matatizo hayo.

    Na Xi Jinping amesisitiza kuwa, viongozi wapya wa kamati kuu ya chama siku zote watakuwa na hisia sawa na wananchi, kuungana na wananchi wakati wa shida na raha, na kufanya juhudi pamoja na wananchi, na kutumia madaraka kwa ajili ya wananchi, na kufanya kazi kwa bidii zaidi, ili kufanikisha mtihani kwa historia na wananchi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako