• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kimbunga cha Bopha chasababisha vifo vya watu 129 nchini Philippines

    (GMT+08:00) 2012-12-05 19:06:45

    Idadi ya vifo kutokana na kimbunga cha Bopha kilicholikumba eneo la kusini mwa Philippines imeongezeka na kufikia 129. Upepo mkali na mafuriko vimeikumba maeneo mbalimbali katika kisiwa cha Mindanao.

    Baraza la kupunguza na kukabiliana na maafa la mkoa huo limesema, hadi kufikia mchana wa leo, idadi ya watu waliofariki mkoani Davao Oriental pekee imefikia 81, wengine 148 wamejeruhiwa, 25 hawajulikani walipo, na wengine 5,737 wakipoteza makazi yao. Kimbunga hicho pia kimesababisha uharibifu wa nyumba kadhaa, majengo, na barabara za mkoa huo. mkoani Compostela Valley, watu 48 wamefariki, idadi hiyo haikuhusisha askari watatu waliofariki wakati wakiwaokoa waathirika wa kimbunga hicho.

    Rais Benigno Aquino III amemwagiza waziri wa usafiri na serikali za mitaa Manuel Roxas kufuatilia hali halisi ilivyo kisiwani Mindanao. Rais Aquino ameahidi kutembelea mikoa ya Compostela Valley na Davao Oriental mapema iwezekanavyo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako