• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • FAO lazitaka nchi mbalimbali ziweke mazingira mazuri ya uwekezaji kwa maendeleo ya kilimo

    (GMT+08:00) 2012-12-07 19:11:53

    Ripoti ya "Hali ya nafaka na kilimo ya mwaka 2012" iliyotolewa jana tarehe 6 na Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa FAO imesema, njia bora zaidi katika kupunguza uhaba wa chakula na kuimarisha hifadhi ya mazingira ni kuongeza uwekezaji wa kilimo na kuhakikisha sifa ya uwekezaji.

    Kwa mujibu wa ripoti hiyo, uwekezaji katika kilimo ni muhimu sana, na mkakati wa uwekezaji huo unapaswa kuwapa kipaumbele wakulima, lakini jambo hilo linazuiliwa na mazingira mabaya ya uwekezaji.

    Ripoti hiyo inaona kuwa, katika nchi nyingi zenye pato dogo, hali nyingi kama vile usimamizi mbaya, utekelezaji mbaya wa sheria, ufisadi wa viongozi, kodi kubwa za vifaa vya kilimo, miundo mbinu mbaya na ukosefu wa huduma kwa umma vijijini yote hayo huathiri vibaya nia ya uwekezaji katika kilimo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako