Serikali ya Philippine leo imesema, idadi ya watu waliokufa kutokana na kimbunga cha Bopha imefikia 647. Wakati huohuo, idara ya taifa ya kukabiliana na kupunguza majanga imesema, watu 1482 wamejeruhiwa na wengine 780 hawajulikani walipo. Idara hiyo imesema kimbunga hicho kimeathiri watu milioni 5.4 katika mikoa 30, wengi wao wakitokea sehemu ya kati na kusini mwa Philippines.
Ripoti iliyotolewa na idara hiyo inasema, hasara ya uharibifu wa miundo mbinu kutokana na kimbunga hicho imefikia dola za kimarekani milioni 84.99.
Kimbunga cha Bopha ni kimbunga chenye nguvu kubwa zaidi kuliko kingine kilichoikumba Philippines kwa mara 16 mapema mwaka huu.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |