• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Barua 1204

    (GMT+08:00) 2012-12-19 15:35:58
    Barua ya kwanza inatoka kwa msikilizaji wetu Chitechi B. Wycliffe wa S.L.P 2812-50100 Kakamega Kenya anaanza kwa kusema kwanza napenda mpokee salamu nyingi kutoka kwangu na kwa familia yangu nzima nikiwa kama msikilizaji wenu wa dhati. Kwa heshima na taadhima kuu napenda kuwapa mkono wa pongezi kwa ubora wa hali ya juu wa vipindi na kukidhi haja za wasikilizaji hapa nchini Kenya.

    Kwa hakika uhusiano kati ya China na Afrika umeendelezwa kwa kasi na kupata mafanikio yanayovutia ulimwenguni. Kwa ujumla msaada wa China kwa Afrika, biashara na uwekezaji wa China barani Afrika umekuwa mkubwa sana na umeinua uchumi wa Afrika. Mambo mengi yamesemwa kuhusu uhusiano uliopo kati ya China na Afrika. Mimi kama msikilizaji wenu nazidi kuwapongeza na kukanusha ukosoaji na lawama za baadhi ya watu duniani juu ya uhusiano uliopo kati ya China na Afrika, pia nashukuru kwa kila barua mnayonitumia.

    Mimi kama mpenda mazingira nimejaribu kuhamasisha wananchi lakini naona kuna upungufu mkubwa kwa watu kutunza mazingira. Ahsanteni sana.

    Sasa ni zamu ya msikilizaji wetu Gulam Haji Karim wa S.L.P 504 Lindi Tanzania, naye anasema natoa salamu za kutimiza miaka 63 kwa Jamhuri ya watu wa China kuanzia viongozi waasisi Bw. Mao Tse Tung, Zhou Enlai. Hivi sasa China imepiga hatua kubwa kimaendeleo, wananchi wote wananufaika na wafanyakazi wanachapa kazi kwa nguvu ili kujiletea maendeleo. Miji mikuu mingi ni miji ya maendeleo, biashara na viwanda vikubwa na vidogo.

    Wakulima nao wanaendeleza kilimo cha kisasa, China inajitegemea kwa chakula na kingine kuuza nchi za nje. Kwa upande wa viwanda vinatengeneza vitu kuanzia peni hadi magari, matrekta na treni, mara mojamoja hupata kuona kuwa katika miji mikubwa ya China inashindana na ya Ulaya. Katika mawasiliano China ina barabara za njia sita mbali ya barabara za juu. Treni za kasi za juu ya ardhi na chini ya ardhi.

    Pamoja na yote China inatoa misaada na mikopo bila masharti yoyote ya kulazimisha au kuweka kikwazo chochote, nchi nyingi za Afrika zimejikomboa kwa msaada mkubwa wa China na mpaka sasa inaendelea kutoa misaada ya kiuchumi na kimaendeleo kwa nchi changa. Naitakia maendeleo makubwa zaidi na pongezi nyingi kwa watu wa China, ahsante sana.

    Tunawashukuru kwa dhati wasikilizaji wetu Chitechi B. Wycliffe, na Gulam Haji Karim kwa barua zenu, kwanza tunakupongeza sana Bw. Chitechi B. Wycliffe kwa kuwa mwanaharakati wa mazingira, ni jambo la kupendeza kwani siku hizi watu wamekuwa hawajali sana wanakata miti ovyo, kwa hiyo ukiendelea kujitahidi na kuhamasisha wengine dunia itakuwa mahali salama kabisa pa kuishi. Kuhusu uhusiano kati ya China na Afrika kwa kweli umepiga hatua kubwa tunaomba uendelee kudumu na tuendelee kusaidiana zaidi na maendeleo pia yanazidi kuwa juu ndio maana China inajaribu kutumia maendeleo yake ili kuzinufaisha nchi za Afrika, ahsante sana.

    Barua ya sasa inatoka kwa msikilizaji wetu Emmanuel Sikabwe wa Bukavu Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. anasema wapendwa watangazaji wa idhaa ya kiswahili ya redio CHINA Mimi ni mwenyekiti wa chama ya wasikilizaji cha redio China kimataifa. Napenda kuwa julisha kwamba huku kwetu mashariki ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kuna habari nyingi muhimu zinazotokea, lakini hatuzisikii mkizitangaza kwenye redio China. Kwa hiyo tuna waomba mtuunge mkono ili tupate kufanya kazi hiyo pamoja tuwe na wapasha habari zenye kutokea huku kwetu DR Kongo. Tunapenda kujuwa hisia yenu kuhusu pendekezo letu, tuna subiri jibu lenu. Asante

    Shukran za dhati msikilizaji wetu Emmanuel Sikabwe kwa barua yako, kwa kweli habari kuhusu Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo huwa tunajitahidi kuzitoa ingawa sio nyingi sana lakini tutajitahidi kuongeza zaidi ili nanyi watu Kongo muweze kujua kinachoendelea huko Kongo kupitia redio yetu, ahsante sana.

    Bw. Paul Ng'ang'a, anasema yeye ni msikilizaji na mpenzi wa vipindi vinavyopeperushwa hewani na Radio China Kimataifa. Na hapa ana suali kwa kituo hiki maarufu.

    Je, nawezaje kupata ufadhili ili nami niweze kujiunga na idara yeyote ile, ili nikasomee lugha ya Kichina na baadaye niweze kuwa mmoja wa watangazaji wa kituo hiki cha Radio China. Nitashukuru nikipata jibu kutoka ofisi yenu na hata nitafurahi kupokea mawaidha yeyote kuhusu jambo hili.

    Kwanza tunakushuru sana msikilizaji wetu Paul Ng'ang'a kwa barua yako fupi, kuhusu suali lako unaweza kujiunga na chuo kilichopo nchini kwako, yaani chuo cha confucious kwani nchini kwako Kenya kipo, halafu ukimaliza mafunzo, kama tunahitaji mfanyakazi unaweza kuomba kwenye redio yetu, ahsante sana.

    Na mwisho tunawasomea ujumbe tuliotumiwa wenye tovuti yetu kwanza ni Bw. Harrison mollel barua pepe yake ni herichizo@hotmail.com anasema mimi napenda kusikiliza idhaa ya Kiswahili ya redio China. naomba mniambie ni lini kunakuwa na kipindi cha kutafuta marafiki. au kama hamna naomba muweke kipindi hicho cha kutafuta marafiki katika radio

    Msikilizaji wetu huyu hakuweka jina ila baruapepe yake ni grover71@ovi.com anasema tunawashukuru kwa vipindi vyenu ambavyo vinatujulisha matukio na tamaduni za wachina

    Tunawashukuru wasikilizaji wetu kwa ujumbe wenu, na kumjibu Bw. Harrison mollel, ni kwamba hapa idhaa ya Kiswahili tuna kipindi cha cheche zetu ambapo kila siku ya Alhamis kuna kipindi cha upo wapi kinachokuwezesha kumtafuta mtu aliyekupotea, tunatumai tutakuwa tumekujibu suali lako, ahsanteni sana.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako