• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Barua 0115

    (GMT+08:00) 2013-01-18 15:29:08
    Barua ya kwanza inatoka kwa waziri wa shida na mipango ya ghafla Sali Bunzali Sali wa Kashishi Kahama Tanzania. Anaanza kwa kusema awali ya yote nitoe shukrani zangu za dhati kwenu redio China Kimataifa. Nimepata fursa fupi ya kutoa maoni yangu katika redio hii. Kama ilivyo ada naomba nianze kwa kumshukuru mwenyezi mungu mwingi wa rehema. Kwa kuweza kunifikiria mimi Sali Bunzali Sali, kabla ya kueleza kile ambacho kimenisukuma kuandika napenda kuushukuru uongozi wote wa CRI.

    Najuwa wasikilizaji wa CRI tuko wengi. lakini mimi nimepata msukumo wa pekee na kuwataka mpokee maoni yangu. Baada ya kusema hayo. Napenda pia kutumia fursa hii kuwashukuru ninyi nyote watangazaji mmoja mmoja na katika umoja wenu. Pia nafanya hivyo nikitambua vyema kwamba. Kama sio nyinyi watangazaji jina langu au majina ya wasikilizaji wenzangu. Tusingeweza kusikilizana kwa kiasi hiki. Pia najuwa Redio China Kimataifa. kulikuwepo na watangazaji wengine ambao hamko nao kwa sasa kutokana na sababu mbalimbali zilizokua ziko nje ya uwezo wenu. Kwa imani yangu mmekuwa na imani na mimi nikiwa kama msikilizaji mpya CRI. Pia nafahamu mimi kama msikilizaji. wapo wasikilizaji wenzangu ambao labda tunakosea katika namna fulani kutuma ujumbe. Ambapo labda tunakosea ujumbe unakuwa uko nje ya utaratibu. Uelewa wenu ndio unasaidia katika kumshauri msikilizaji aliyekosea ujumbe akatuma tofauti na kile kinacho zungumziwa.

    Dhana ambayo kila ninapokaa na kufikiria. Huwa inanirejesha kuikumbuka idhaa ya Kiswahili ya CRI kwa kipindi chake cha usiku. muda unapokaribia. Hunilazimu nikae karibu na redio ili nisikilize habari za ulimwengu. Nina kila sababu ya kuishukuru CRI kwa kazi zake sio za kubahatisha. Mimi nitumie nafasi hii ya kuweza kuzungumza machache katika idhaa ya Kiswahili ya CRI.

    Maoni yangu. napenda matangazo yenu yawe na vipindi vitatu kwa siku. Asubuhi, mchana, na jioni, hapo ndipo wasikilizaji tutaweza kujivunia na matangazo ya CRI. Mimi sitakuwa na sababu zaidi ya kuwashukuru kwa kazi yenu ni nzuri. Mnayoyafanya yote ni mazuri kwangu, Niwatakie kheri ya mwaka mpya uwe na mafanikio zaidi, nitangulize maombi yangu kwa mungu. Mzidi kuwa na ushirikiano na sisi wasikilizaji wenu. Mungu ibariki CRI na watangazaji wake. Ahsante.

    Tunakushukuru kwa dhati msikilizaji wetu Sali Bunzali Sali kwa barua yako, tunapokea pongezi tukiwa na wingi wa matumaini na furaha, kwani kama sio nyinyi wasikilizaji, pia redio hii isingekuwepo. Pia tunapenda kukwambia kuwa matangazo yetu tunarusha kwa vipindi vitatu, yaani asubuhi, mchana na usiku, na wakati wa mchana mara nyingi Dj Moss ndio anaongoza jahazi, mwisho nasi pia tunakutakia heri na mafanikio ya mwaka mpya, asante sana.

    Barua ya sasa inatoka kwa msikilizaji wetu Epafra Stanley Deteba. Anasema awali ya yote, heri ya mwaka mpya marafiki zangu wapendwa wa CRI, zaidi napenda kuwashukuru sana idhaa ya kiswahili redio China kimataifa kwa moyo wa dhati wa kutujali sisi wasikilizaji wenu toka mwaka uliopita wa 2012, pia nawashukuru sana kwa zawadi mliyo nitumia nimeipokea kwa furaha sana, pia katika mwaka huu wa 2013 nitaendelea kushirikiana nanyi ikiwa ni kwa njia ya barua pepe au hata kwa njia ya sanduku la posta, furaha yangu ni kuitegea sikio CRI, pia nampa pongezi zangu za dhati mama Chen kwa tuzo aliyoipata, vile nawatakia wafanyakazi na watangazaji wote wa CRI katika mwaka huu wa 2013 maisha mema na yenye furaha tele, mimi nawapenda sana, ahsante sana.

    Nasi tunakushukuru kwa dhati msikilizaji wetu Epafra Stanley Deteba kwa barua yako, kwanza napenda kupokea pongezi zako kuhusu tuzo ya urafiki kati ya China na Afrika. Pia tunapenda kuwaambia wasikilizaji wetu kuwa mwaka huu tutaendelea kujitahidi kuboresha zaidi matangazo yetu pamoja na vipindi, mwisho tunawaomba wasikilizaji wote muendelee kusikiliza matangazo yetu na kutoa maoni na mapendekezo, ahsante sana.

    Na sasa tunawaletea ujumbe tuliotumiwa na wasikilizaji wetu kupitia kwenye tovuti yetu kwanza ni kutoka kwa msikilizaji wetu Serge Muzusangabo barua pepe yake ni sergemasu@yahoo.fr anasema hamjambo CRI na wasikilizaji wote, nawasalimu kutoka mashariki mwa jamhuri ya kidemokrasia ya Congo, ninapenda sana vipindi vyenu hasa kile chajifunze kichina.

    Ujumbe mwingine unatoka kwa msikilizaji wetu Chalamila Fred Chelestino wa Sanduku La Posta 21 k, anasema ujumbe ni kuhusu habari ya "jeshi la Syria lawasaka wapiganaji kutoka Uturuki na nchi za ghuba "

    Tabia ya mataifa ya magharibi waache kuingilia migogoro isiyo wahusu jana kwa Gaddafi leo kwa Bashar Al-Asadi je kesho watakuwa kwa nani?

    Davis Mpuso wa S.L.P 370 Sekomu Lushoto Tanga Tanzania anasema siku za jumamosi na jumapili matangazo hayapatikani kupitia KBC. Muda huo wa saa nne usiku sasa sijui kama yanasogezwa mbele ama la. wazo langu bado nasisitiza kwamba mtafute radio washirika hapa TANZANIA wenye mawanda mapana ya kurusha matangazo yao hapa nchini. Msikilizaji wenu. nawatakia kazi njema.

    Tunawashukuru kwa dhati wasikilizaji wetu wote waliotutumia ujumbe kwenye tovuti yetu, lakini tukimjibu Bwana Davis Mpuso kuhusu kutopatikana matangazo kwa siku za Jumamosi na Jumapili, tutajitahidi kufuatilia tuone tatizo ni nini, pia tunaendelea na jitihada zetu ili tuweze kurusha matangazo Tanzania, lakini wenzetu TBC wanatuangusha, hadi leo hawajatupa jibu muafaka, hata hivyo msikate tamaa sisi tutaendelea kujitahidi ili tuhakikishe nanyi watanzania hususan wa Bara pia mnafaidika na matangazo yetu, ahsanteni sana.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako