• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Xi Jinping asisitiza kuwa ni lazima kupambana na ufisadi kwa njia ya ufanisi na ya kisayansi

    (GMT+08:00) 2013-01-23 19:32:00

    Katibu mkuu wa Kamati kuu ya chama cha kikomunisti cha China CPC Bw. Xi Jinping jana tarehe 22 amesisitiza kuwa, ni lazima kupambana na ufisadi kwa njia ya kisayansi yenye ufanisi, kuimarisha kazi ya kuzuia na kusimamia matumizi ya madaraka, kufunga matumizi ya madaraka ndani ya kizimba cha utaratibu wa sheria, ili kuunda utaratibu wa kutoa adhabu wa kuwafanya watu kutothubutu kufanya ufisadi, kuunda utaratibu wa kuzuia watu kufanya ufisadi, na utaratibu ambao ni vigumu kufanya ufisadi.

    Bw Xi ametoa hotuba kwenye mkutano wa kamati kuu ya nidhamu ya Chama cha Kikomunisti cha China akisisitiza kuwa, chama hicho kikiwa chama tawala kinakabiliwa na changamoto kubwa ya kupambana na ufisadi, ni lazima kupata ufanisi halisi wa mapambano dhidi ya rushwa ili kuongeza imani ya wananchi kwa chama na serikali yao.

    "Wanachama wengi na makada wengi hawana tatizo la ufisadi, hata hivyo tunatakiwa kutambua kwamba, hali ya uzembe na ufisadi inaonekana mara kwa mara katika nyanja kadha wa kadha, na baadhi ya matukio ya kukiuka vibaya nidhamu yameleta athari mbaya kwenye jamii, na vita dhidi ya ufisadi bado inakabiliwa na changamoto kubwa, na haijawaridhisha wananchi. Juhudi za kupambana na ufisadi zinatakiwa kuendelezwa kithabiti bila kulegalega, adhabu kali zinatakiwa kutolewa kwa watu watakaotoa au kupokea rushwa. Ni lazima kung'oa mizizi yote ya ufisadi na kupata ufanisi halisi utakaoweza kuongeza imani ya wananchi kwa chama na serikali yao."

    Bw Xi amesisitiza kuwa wanachama hawaruhusiwi kutumia nafasi zao kujitafutia maslahi yoyote binafsi na haki maalum na yeyote anayehusika na ufisadi ataadhibiwa.

    "Utawala wa kufuata nidhamu na maadili ndio unaoweza kuaminiwa na wananchi, kutumia madaraka kwa ajili ya umma ndiyo kunaweza kuongeza imani ya wananchi kwa chama na serikali. Kwa hiyo tunatakiwa kujenga mfumo wa kutoa adhabu na kuzuia vitendo vya ufisadi, kutoa elimu ya kupambana na ufisadi, na kuweka mazingira safi. Kukamilisha mfumo wa kuzuia na kusimamia matumizi ya madaraka, kutunga sheria za kupambana na ufisadi, na kuzifanyia mageuzi sekta zenye matatizo mengi ya ufisadi. Viongozi wa ngazi mbalimbali wanapaswa kukumbuka, mtu yeyote hana madaraka ya juu nje ya sheria, kutumia madaraka kwa mtu yeyote ni kwa ajili ya kuwahudumia wananchi, kuwawajibika na kuwanufaisha wananchi, hivyo ni lazima asimamiwe na wananchi kwa hiari."

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako