• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yashikilia njia ya kujiendeleza kwa amani

    (GMT+08:00) 2013-01-28 18:06:30

    Mkutano wa mwaka wa baraza la mabunge ya nchi za Asia na Pasifiki APPF unafanyika leo tarehe 28 huko Vladivostok, Russia. Katika mkutano huo, spika wa bunge la umma la China, Wu Bangguo, amesisitiza kuwa, kushikilia njia ya kujiendeleza kwa amani ni chaguo la kimkakati lililofanywa na China kwa kufuata mkondo wa maendeleo wa zama za hivi sasa na maslahi ya kimsingi ya China, na msimamo huo hautabadilika kutokana na mabadiliko ya uwezo wa nchi na hadhi yake ya kimataifa.

    Baraza la APPF lililoanzishwa mwaka 1993 lina nchi wajumbe 27 zikiwemo China, Russia na Marekani. Mkutano wa mwaka wa baraza hilo ambao ni wa ngazi ya juu unaotoa maamuzi unafanyika kila mwaka kwa zamu katika pande mbili za bahari ya Pasifiki. Habari zinasema kuwa, mkutano huo wa siku tatu utajadili kuhusu masuala ya usalama wa kikanda, uchumi na biashara, pamoja na ushirikiano wa kikanda.

    Katika mkutano huo, Spika Wu Bangguo alifafanua msimamo wa China katika masuala makubwa kuhusu sehemu ya Asia na Pasifiki kujiendeleza kwa amani. Anasema:

    "Tunapaswa kuacha wazo la vita baridi, kuheshimu mamlaka na maslahi muhimu ya kila upande, kuhimiza kuanzishwa kwa utaratibu wa usalama wa kikanda ulio wa haki na wenye ufanisi; kuhimiza ushirikiano wenye ufanisi katika sekta za teknolojia mpya na ya kiwango cha juu, utengenezaji wa kisasa wa bidhaa, kubana matumizi ya nishati na kulinda mazingira, maliasili za nishati, pamoja na kilimo cha kisasa, kupinga vitendo vya kujilinda vya aina mbalimbail, na kuhimiza biashara na kuhakikisha uwekezaji unafanyika bila vizuizi vyovyote, na utandawazi wa uchumi wa kikanda. Pia kuheshimu aina nyingi za ustaarabu, kuheshimu njia za kujiendeleza zilizochaguliwa na watu wa nchi mbalimbali, kuhimiza nchi zenye ustaarabu na mifumo tofauti ya jamii ziwasiliane na kufundishana, ili kusukuma mbele maendeleo ya pamoja ya nchi za Asia na Pasifiki. "

    Spika Wu amesema mabunge yanafanya kazi muhimu katika mambo ya siasa na maslahi ya nchi mbalimbali. Mabunge ya nchi wajumbe wa baraza la APPF yanatakiwa kuhimiza na kuunga mkono serikali zao kutekeleza sera za kidiplomasia zinazosaidia zijiendeleze kwa amani, kunufaishana na kupata maendeleo kwa pamoja. Anasema:

    "China imepata mafanikio yanayofuatiliwa na dunia, lakini pia inakabiliwa na matatizo na changamoto mbalimbali. Hivi sasa kujiendeleza ni njia muhimu kwa China kukabiliana na changamoto zote, hivyo itatilia mkazo zaidi kazi za kujiendeleza, kufuata kwa makini mikakati ya kufanya ushirikiano wa kunufaishana ili kupata maendeleo kwa pamoja, huku ikijitahidi kufungua mlango zaidi katika sekta mbalimbali."

    Wakati wa mkutano huo, mwenyekiti wa Kamati ya Shirikisho la Russia ambayo ni nchi mwenyeji wa mkutano huo Bi Valentina Matviyenko amezitaka pande zote zinazohusika kufanya juhudi kwa pamoja ili kuhimiza baraza hilo lipate maendeleo makubwa zaidi. Anasema:

    "Hii ni mara ya pili kwa Russia kuandaa mkutano huu. Baraza la APPF ni shirika lenye ushawishi mkubwa zaidi kati ya mabunge ya nchi mbalimbali katika sehemu ya Asia na Pasifiki. Katika miaka 20 iliyopita, baraza hili limejadili masuala mbalimbali makubwa yanayohusu maendeleo ya dunia na ya kikanda. Naamini kuwa mkutano huu utasaidia kutunga mwongozo wa utekelezaji wa hatua zitakazochukuliwa katika siku za baadae."

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako