Vikosi vya jeshi la Algeria vimeshambulia kundi la watu wanaoshukiwa kuwa ni wapiganaji katika kijiji cha Mazar, mkoani Tizi Ouzou, kilomita 130 kutoka magharibi mwa mji mkuu wa Algeria, Algiers, na kumwua mpiganaji mmoja, ambaye ni wa kwanza kuuawa mkoani humo katika mwaka huu.
Jumapili iliyopita, watu wenye silaha waliwashambulia walinzi wa kambi ya jeshi la manispaa wenye majukumu ya kulinda bomba la gesi mkoani Bouira, na kusababisha vifo vya walinzi watatu.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |